Katika harakati za kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya watoto wa kike, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limeanzisha programu maalum ya mchezo wa mpira wa miguu au kabumbu katika kambi ya wakimbizi ya Za’atari nchini Jordan ili kutoa fursa kwa watoto hao wa kike na wasichana kufanya mazoezi.