Haki za binadamu

Serikali ya Kenya lindeni watetezi wa mazingira UN

Serikali ya Kenya imeshauriwa kuchukua hatua za  haraka kulinda watetezi wa mazingira  ambao sasa wanakabiliwa na vitisho pamoja na udhalilishwaji.

Raia wa Sudan Kusini asimulia alivyobakwa baada ya mumewe kuuawa

Hali bado si shwari kwenye jimbo la Unity nchini Sudan Kusini, jambo linalofanya maelfu ya raia wa kukimbia mapigano huku wakikumbwa na madhila ikiwemo kubakwa. 

Algeria acheni kuwatimua kwa pamoja wahamiaji:UN

Umoja wa Mataifa leo umetoa wito kwa serikali ya Algeria kusitisha vitendo vya kuwafukuza kwa pamoja wahamiaji hususani kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Ingawa idadi kamili ya waliotimuliwa haijajulikana inaaminika ni maelfu ya wahamiaji.

Mauaji ya watoto Burundi katu hayakubaliki:UN

Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulio lililotokea mkoani Cibitoke nchini Burundi na kukatili Maisha ya watu 25 wakiwemo watoto 11.  Tupate maelezo zaidi na Grace Kaneiya

Chonde chonde Sudan ruhusuni rufaa ya Noura: UN women/UNFPA/UNOSAA

Aozwa kwa lazima, akatoroka  , nduguze wakamrejesha kwa nguvu kwa mumewe ambaye alimbaka, na kwa kushindwa kuvulia hilo akamchoma kisu mumewe na kumua, sasa Noura hassan kutoka Sudan anakailiwa na hukumu ya kifo, mashirika ya Umoja wa Mataifa, raia wa sudan na wanaharakati wa haki za wanawake na wasichana wanataka aruhusiwe kukata rufaa.

Katu hatukubali watoto milioni 250 wawe mbumbumbu- UN

Elimu yasalia ndoto kwa watoto wengi duniani hususan wa kike, sasa hii leo vijana wenzao wamechukua hatua madhubuti.

Wanawake warohigya: Baada ya kubakwa sasa ni wajawazito

Idadi kubwa ya wanawake na wasichana 40,000 wakimbizi wa kirohingya ambao ni wajawazito hivi sasa, walipata hali hiyo baada ya kubakwa.

Uamuzi wa mahakama Tanzania ni ushindi kwa umma- Balile

Nchini Tanzania hii leo Mahakama Kuu kanda ya Mtwara imezuia kwa muda kuanza kwa matumizi ya kanuni mpya za maudhui ya mtandao nchini humo.

Jukwaa la mawasiliano kati yetu ni muarobaini- Dkt. Mwakyembe

Mazingira yalivyo hivi sasa ni lazima kuwepo na mawasiliano ya mara kwa mara kati ya serikali na vyombo vya habari.

Mambo ni magumu lakini tusikate tamaa- Mukajanga

Nchini Tanzania Baraza la Habari nchini humo, MCT, limesema maudhui ya mwaka huu ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari yamekuja wakati muafaka ambapo uhuru wa vyombo vya habari unabinywa kimataifa hadi kitaifa.