Afya

Juhudi za kuimarisha uzazi salama huko Tanzania

White ribbon alliance ni mungano wa kimataifa wa watu na mashirika uloundwa kuhamasisha wananchi juu ya haja ya kuwepo na afya nzuri na usalama kwa wanawake wote wajazito na wanapojifungua pamoja na watoto wanaozaliwa.

Msaada wa kwanza wa Zambia kwa WFP unasaidia kupunguza upungufu wa chakula.

Program ya Chakula Duniani WFP, imepongeza mchango wa kwanza kabisa kutoka kwa serekali ya Zambia, ambao utawawezesha maelfu ya wa Zambia kupokea msaada muhimu wa chakula baada ya Septemba.

Kupunguka kwa mazao 2007 kutasababisha upungufu wa chakula

Shirika la Chakula Duniani FAO, imeripoti kwamba upungufu wa kiwango cha uzalishaji nafaka mwaka huu katika mataifa maskini duniani huwenda kukapelekea kuwepo na hali ngumu ya akiba ya chakula, ambapo mataifa 28 yatakabiliwa na upungufu mkubwa zaidi wa chakula.

Umoja wa Mataifa waomba msaada kupambana na utapia mloo

Na ripoti yetu ya pili kwa hii leo ni kwamba mashirika ya Umoja wa Mataifa huko Kenya yalitangaza wiki hii kwamba wanahitaji dola milioni 32 kutoka kwa wafadhili ili kuweza kupunguza kiwango cha utapia mloo ambacho wamesema kimefikia hali ya hatari miongoni mwa watoto chini ya miaka mitano ndani ya makambi ya wakimbizi. ~

Serekali za eneo na UM zakubaliana 'ramani' ya kupambana na tatizo la njaa Pembe ya Afrika

Wajumbe wa Serekali za Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya Usomali na Uganda pamoja na wawakilishi wa UM walikutana kwa mazungumzo ya siku mbili mjini Nairobi (Kenya) wiki hii na walikubaliana kukabili kipamoja vyanzo vyenye kuchochea matatizo ya njaa katika maeneo ya Pembe ya Afrika.

Operesheni inayoungwa mkono na UM itawakinga watoto milioni 2 Zambia dhidi ya shurua

Kuanzia tarehe 09 hadi 14 Julai mashirika ya UM juu ya maendelo ya watoto UNICEF na afya WHO yatajumuika kuhudumia kipamoja chanjo dhidi ya shurua kwa watoto milioni 2 nchini Zambia.

NKM atahudhuria Mkutano Mkuu wa AU Ghana

Naibu KM (NKM) Asha-Rose Migiro anatazamiwa kuelekea Afrika na Ulaya mwisho wa wiki. NKM atamwakilisha KM kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) utakaofanyika mwanzo wa Julai mjini Accra, Ghana. Kabla ya hapo NKM Migiro ataelekea Vienna, Austria kutoa hutuba ya ufunguzi kwenye \'Jopo la 7 la Dunia la Uvumbuzi Mpya Ziada wa Shughuli za Serikali\'. Baada ya hapo ataelekea Guinea-Bissau, ikiwa ziara ya kwanza rasmi ya KM au NKM tangu taifa hilo kujiunga na UM.

Ukame wazusha upungufu mkubwa wa chakula Lesotho

Ripoti mpya ya Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) pamoja na Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) imedhihirisha ya kwamba khumsi moja ya idadi ya watu nchini Lesotho, yaani watu 400,000, inakabiliwa na tatizo hatari la ukosefu mkubwa wa chakula, kufuatia ukame mbaya uliotanda karibuni kwentye taifa hilila kusini ya Afrika. Kwa mujibu wa taarifa UM hali hii haijwahai kuhushudiwa kieneo kwa muda wa miaka 30 ziada. Jumuiya ya kimataifa pamoja na wahisani wa kimataifa, wamehimizwa kushirikiana kipamoja kupeleka misaada ya dharura ya kihali, na pia misaada ya chakula, kwa Lesootho na katika mataifa jirani yanayokabiliwa na tatizo la ukame mbaya ili kunusuru maisha ya mamilioni ya raia wa kusini ya Afrika.

Hali ya chakula katika Zimbabwe inaregarega; UNICEF kusaidia kuchanja watoto dhidi ya polio

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF) pamoja na mashirika wenzi yameanzisha kampeni ya pamoja ya kuwapatia watoto milioni 2 nchini chanjo dhidi ya maradhi ya kupooza (polio) katika Zimbabwe, hasa ilivyokuwa asilimia kubwa ya raia inakabiliwa na matatizo yanayosababishwa na kuporomoka kwa maendeleo ya uchumi kitaifa.

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon amepokea kwa moyo thabiti maafikiano yaliofikiwa na viongozi wa kundi la G-8 kwenye mji wa Heiligendamm, Ujerumani ambapo walikubaliana kuchukua hatua za mapema, na zenye nguvu kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani, na kuahidi kutumia mfumo wa Umoja wa Mataifa (UM) katika kuitekeleza miradi hiyo.