Afya

Msanii wa Tanzania ashirikiana na UNFPA kuhudumia uzazi bora

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Muongezeko wa Watu Duniani (UNFPA)Thoraya Obaid alikumbusha kwenye risala yake ya karibuni kwamba umma wa kimataifa umeingia kwenye karne ambayo hawatovumilia tena vifo vya mama wakati wa kuzaa. Alisema UNFPA itajitahidi kufanya kila iwezalo, kwa ushirikiano na nchi husika, kuhakikisha janga hili linakomeshwa kote duniani.

Utekelezaji wa MDG katika sekta afya mkoani Tabora, Tanzania (Sehemu ya Pili)

Katika makala iliopita tuliripoti kwamba karibuni nilipata fursa ya kutembelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nilipokuwa huko nilizuru moja ya vijiji kumi vilivyochaguliwa rasmi na UM barani Afrika kuwa vjiji vya milenia.

Juhudi za kukamilisha MDGs Tabora, Tanzania

Hivi karibuni nilizuru Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nilipatiwa fursa ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliohusishwa kwenye huduma za utekelezaji wa ile miradi ya UM ya inayoambatana na Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

Mkutano muhimu wafanyika London kuzuia vifo vya mama wazazi

Taarifa za UM zimeripoti kwamba wajumbe zaidi ya 1,800 wanaohusika na maandalizi ya sera za kitaifa, pamoja na wataalamu, wawakilishi wa mashirika yasio ya kiserekali (NGOs), wanaharakati wanaogombania haki za wanawake na vile vile watu mashuhuri kadha wa kadha kutoka nchi 100 ziada walikusanyika karibuni mjini London kwenye mkutano maalumu ulioahidi kulipa “umuhimu, wa kiwango cha juu, suala la kuboresha afya ya mama wazazi." Kadhalika wajumbe hawo waliahidi kuliingiza suala la kuboresha huduma za uzazi kwenye ajenda za miradi ya afya, kitaifa, kikanda na kimataifa.

UM umeshirikiana na Sudan kuchanja watoto dhidi ya polio

Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF) yakijumuika na Wizara ya Afya ya Sudan yameendeleza huduma za pamoja za kuwachanja polio watoto wachanga katika Sudan kuanzia tarehe 23 hadi 25 Oktoba.

Hapa na pale

Rachel Mayanja, Mshauri Maalumu wa KM kuhusu Masuala ya Kijinsia na Maendeleo ya Wanawake amependekeza kwa jamii ya kimataifa kubuniwe kanuni za kukabiliana na vitendo haramu vya kutumia mabavu na kujamii kwa nguvu wanawake kwenye mazingira ya vita, na alitaka vitendo hivi vitafsiriwe kama uvunjaji sheria wa kiwango cha juu wenye kuvuka mipaka ya maadili ya kiutu.~

Wawakilishi wa KM wakutana na Raisi Kabila kusailia usalama katika Kivu

Mnamo mwanzo wa wiki, Mwakilishi Maalumu wa KM katika Jamhuri ya Kideomkrasi ya Kongo (DRC), William Swing akifuatana na Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Amani vya UM vya MONUC, Jenerali Boubacar Gueye Walikutana kwa mashauriano na Raisi Joseph Kabila kwenye mji wa Goma, kaskazini-mashariki ya nchi, kusailia hali ya usalama katika jimbo la Kivu Kaskazini, eneo ambalo karibuni lilizongwa na hali ya mapigano baina ya vikosi vya Serikali na wanajeshi waasi walio’ongozwa na Jenerali Mtoro Laurent Nkunda.

WHO yatoa onyo la kutahadharisha mfumko wa kipindupindu Usomali

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti watu saba karibuni walikutikana kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu katika Usomali kusini. Maradhi haya yanaonekana kuibuka tena nchini miezi mitatu tu baada ya kuua zaidi ya watu 1,100.

Hapa na pale

Tarehe 16 Oktoba huadhimishwa na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) pamoja na aila nzima ya UM kuwa ni ‘Siku ya Chakula kwa Wote Duniani’. Siku hii hutumiwa kuwazindua walimwengu ya kwamba watu milioni 854 bado wanaendelea kuteswa na kusumbuliwa, kila siku, na tatizo sugu la njaa na ukosefu wa chakula, idadi ya waathiriwa ambayo inazidi kukithiri kwa sababu ya mifumo dhaifu ya kilimo, ugawaji usiotosheleza wa chakula, uwezo usiofaa wa kuhifadhia chakula, na vile vile kutokana na hali ya vurugu na mapigano, mazingira ambayo hukwamisha huduma za kilimo kwenye maeneo husika.

Juhudi za kupambana na VVU/UKIMWI Tanzania

Mnamo mwaka 2000 jumuiya ya kimataifa ilikubaliana kuchukua hatua za pamoja ili kupunguza ufukara na umasikini duniani, angalau, kwa nusu, mwaka 2015 utakapowasili, hususan katika mataifa yanayoendelea.