Afya

Watoto 67,000 kuchanjwa dhidi ya surau Ituri DRC-UNICEF

Wahudumu wa afya nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF wanakimbizana na muda katika kampeni ya chanjo kwenye jimbo la ituri Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo baada ya kuzuka mlipuko wa surua uliosababisha karibu vifo 2000 nchi nzima tangu mwanzo wa mwaka huu huku waathirika wengi wakiwa ni watoto wa chini ya miaka mitano.

Wakati wa kuchukua hatua ni sasa wanawake na wasichana hawawezi kusubiri haki zao:UN

Wakati idadi ya watu duniani ikikadiriwa kuongezeka na kufikia bilioni 9 mwaka 2050 Umoja wa Mataifa imezitaka nchi kuzingatia uwiano kati ya ongezeko la idadi ya watu na maendeleo

IOM na Japan wapiga jeki juhudi za kuzuia magonjwa

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM na serikali ya Japan wamezindua mradi wa pamoja kwa mwaka mmoja kwa ajili ya kusaidia watu wanaokabiliwa na milipuko ya magonjwa, majanga ya asili na wanaorejea nchini Burundi.

Mazao ya kilimo yanatarajiwa kupunguza bei ya vyakula katika muongo mmoja ujao licha ya hali ya sintofahamu katika siku zijazo-FAO

Mahitaji ya bidhaa za kilimo yanatarajiwa kukua kwa asilimia 15 katika kipindi cha muongo mmoja ujao huku, ukuaji wa uzalishaji wa bidhaa za kilimo ukitarajiwa kuongezeka kwa kasi zaidi na kusababisha mfumko wa bei. Nayo bei ya bidhaa muhimu za kilimo ikitarajiwa kusalia katika viwango vya sasa au kushuka chini kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo na lile la chakula na kilimo duniani, FAO.

Ukosefu wa usalama unaweka raia hatarini ya kuambukizwa magonjwa ikiwemo ebola-IOM

Machafuko mapya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC eneo ambalo linajizatiti kukabiliana na mlipuko unaoshuhudiwa wa ebola umesababisha vifo vya takriban watu 160 na kusababisha mamia kufurushwa na hivyo kufanya hali ya sasa kuwa mbaya zaidi katika kukabiliana na dharura ya kiafya.

Ugonjwa wa homa ya nguruwe unaendelea kusambaa Asia-FAO

Ugonjwa wa homa ya nguruwe au African Swine Flu, ASF,  unaoathiri nguruwe unaendelea kuenea Asia mashariki na kusini mashariki na kuweka hatarini mfumo wa kuingiza kipato na uhakika wa chakula kwa mamilioni ya watu hususan wakulima wanaofuga nguruwe.

UN yalaani vikali shambulio la bomu Kabul

Watoto kadhaa ni miongoni mwa waliojeruhiwa katika shambulio la bomu kwenye jengo la serikali hii leo mjini Kabul nchini Afghanistan ambalo limetokea karibu na shule kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF.

Wahudumu wa afya na serikali Uganda wanafanya kazi nzuri kudhibiti Ebola:WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limewapongeza wahudumu wa afya na wizara ya afya ya Uganda kwa hatua za haraka na maandalizi ya kupambana na mlipuko wa Ebola uliozuka hivi karibuni nchini humo. 

Sasa mwelekeo ni sahihi kutokomeza ugonjwa wa vikope mwaka 2020

Idadi ya watu walioko hatarini kuugua ugonjwa wa vikope, ugonjwa ambukizi unaoongoza duniani kwa kusababisha upofu imepungua kwa asilimia 91, limesema shirika la afya ulimwenguni, WHO.
 

Chonde chonde wasafiri pateni chanjo dhidi ya Surua- WHO

Kufuatia ongezeko la hivi karibuni la visa vya ugonjwa wa surua katika maeneo mbalimbali duniani hata katika nchi zilizoendelea,  shirika la afya ulimwenguni limetoa angalizo hususan kwa wasafiri kupata upya chanjo dhidi ya ugonjwa huo iwapo hawana uhakika kama waliwahi kupatiwa au la.