Afya

WHO inasema homa ya mafua ya H1N1 imegundiliwa kuenea zaidi Ulaya ya Mashariki kwa sasa

Mataifa ya Ulaya ya kati na mashariki yameripotiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa ndio maeneo ya ulimwengu yaliosumbuliwa zaidi sasa hivi na maambukizo ya homa ya mafua.

"Ukomeshaji wa janga la H1N1 ulimwenguni huenda ukachukua mwaka", ameonya Mkuu wa WHO

Dktr Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kwenye mahojiano mjini Geneva na gazeti la Le Temps, Ijumanne alinakiliwa akisema janga la homa ya mafua ya H1N1 halitofanikiwa kudhibitiwa kikamilifu mpaka mwaka 2011.

EU imechangisha Yuro milioni 5.5 kuisaidia UNRWA kuimarisha afya bora kwa wakazi wa Tarafa ya Ghaza

Ijumatatu, Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza kufadhilia msaada wa Yuro milioni 5.5 kulipa Shirika la UM Linalofarajia Misaada ya Kihali kwa WaFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA) uliokusudiwa kuhudumia miradi ya afya na mazingira safi kwenye Tarafa ya Ghaza.

Mkuu wa UNICEF anajiandaa kumaliza kazi mapema

KM Ban Ki-moon, ametangaza taarifa ya masikitiko yenye kueleza Ann Veneman, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) kwamba hana azma ya kuendelea kazi tena baada ya muda wake kumalizika.

Mashirika ya UM yajihusisha Kenya kudhibiti mripuko wa kipindupindu Turkana Mashariki

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti Alkhamisi jioni kwamba taasisi kadha za UM zinazohudumia misaada ya kiutu, hivi sasa zinajitahidi kuipatia Serikali ya Kenya misaada ya dharura inayohitajika kupambana na mripuko wa maradhi ya kipindupindu, yaliozuka kwenye eneo la kaskazini-magharibi, ambapo tumearifiwa watu karibu 30 walifariki kutokana na ugonjwa huo, kwenye zile sehemu za mbali zenye matatizo kuzifikia.

Ripoti ya Malaria Duniani kwa 2009 yachapishwa na WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO), leo limetangaza Ripoti ya 2009 juu ya Malaria Duniani. Ripoti ilieleza kwamba muongezeko wa misaada ya fedha, mnamo miaka ya karibuni, kuhudumia malaria, umeyawezesha mataifa kadha kufanikiwa kudhibiti maradhi,

UM yathibitisha robo tatu ya vifo vya maafa duniani husababishwa na majanga ya kimaumbile

Margareta Walhstrom, Mjumbe Maalumu wa KM anayehudumia Mpango wa Kupunguza Athari za Maafa amenakiliwa akisema hali ya hewa mbaya kabisa iliojiri ulimwenguni, katika miezi 11 iliopita, ndio matukio yaliosababisha asilimia 75 ya vifo vinavyoambatana na majanga na maafa ya kimaumbile.

Hatua ziada zatakikana dhidi ya matumizi ya tumbaku duniani, inahimiza WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza ripoti mpya inayoeleza kwamba licha ya kuwa idadi kubwa ya umma wa kimataifa huhifadhiwa na zile sheria za kupiga marufuku uvutaji sigara kwenye mazingira ya umma, hasa katika 2008, juu ya hayo tumearifiwa kwamba bado tutahitajia kuchukua hatua ziada za dharura, za kuwalinda watu na maradhi pamoja na vifo vinavyoletwa na athari za moshi wa sigara.

Mradi wa DOTS wafanikiwa kutibu TB watu milioni 36

Katika miaka 15 iliopita, watu milioni 36 wanaripotiwa walitibiwa, kwa mafanikio, maradhi ya kifua kikuu, au TB, ulimwenguni, kwa kutumia utaratibu mkali wa kuhudumia afya bora uliotayarishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

UM inahimiza kujumuishwa kwenye miradi ya MDGs mahitaji ya walemavu na walionyimwa uwezo

Kama mlivyosikia kwenye taarifa za habari wiki hii, kwamba Alkhamisi ya tarehe 03 Disemba (2009) iliadhimishwa hapa Makao Makuu ya UM, kuwa ni Siku ya Kimataifa kwa Watu Walemavu na Wenye Kunyimwa Uwezo wa Kimaumbile.