Afya

KM asihi "vitendo vya mabavu na vurugu" Ghaza visitishwe, haraka.

KM Ban Ki-moon alizungumza na waandishi habari leo adhuhuri ambapo alisihi Israel na ‘Hamas’ kukomesha, haraka, vitendo vyote vya kutumia mabavu katika Tarafa ya Ghaza, na kuchukua hatua zote zinazohitajika kuwaepusha raia na hatari ya kujeruhiwa na mashambulio:~

Ofisa mkaazi wa WHO anasema "hali ni ngumu tangu mashambulio kuanzishwa Ghaza"

Leo asubuhi tulipata taarifa ziada kutoka Mahmoud Daher, Ofisa wa Afya anayewakilisha Shirika la Afya Duniani (WHO) katika Ghaza, ambaye alihojiana, kwa kutumia njia ya simu, na Samir Imtair Aldarabi, mwanahabari wa Idhaa ya Kiarabu ya Redio ya UM. Daher alielezea hali ilivyo sasa hivi katika Ghaza, kama ifuatavyo:~

Mashirika ya UM yameanzisha kampeni ya kunusuru maisha kwa watoto wachanga na wanawake Usomali

Mashirika ya UM juu ya afya duniani, WHO, na huduma za maendeleo ya watoto, UNICEF, yameanzisha kampeni ya kuchangisha mamilioni ya dola zitakazotumiwa kwenye miradi ya kunusuru maisha ya watoto milioni 1.5, walio chini ya umri wa miaka mitano katika Usomali, pamoja na kuwasaidia wanawake wa umri wa kuweza kuzaa, yaani baina ya miaka 15 hadi 49, kujidhibiti kiafya.

Takwimu ziada juu ya Zimbabwe na kipindupindu

Takwimu mpya kuhusu mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika Zimbabwe, zilizosajiliwa na kuthibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mnamo tarehe 25 Disemba zinaonyesha idadi ya wagonjwa wa maradhi hayo siku hiyo ilikuwa 26,497, wakati jumla ya vifo vilirikodiwa ilifikia 1,518.~

UM inakhofia homa ya Ebola imeibuka tena katika JKK

Maradhi yanayotiliwa shaka kuwa ni ya homa ya Ebola, yameripotiwa kuibuka katika JKK, kwenye jimbo la Occidental Kasai, na kuuwa watu tisa kufuatia maambukizo ya wagonjwa 92.

Vijana wanaoishi na VVU Namibia/Tanzania wahitajia mchango wa kitaaluma skulini mwao

Matokeo ya utafiti wa karibuni, uliodhaminiwa na UM kuchunguza mahitaji ya wanafunzi vijana na watoto wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika mataifa ya Namibia na Tanzania, yameonyesha mara nyingi kundi hili dhaifu kiafya, hunyimwa misaada wanayohitajia kujiendeleza kiilimu.

Misaada ya dharura kwa waliong'olewa makazi imewasili Dungu

Malori matano ya Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) yaliobeba tani 23 za misaada ya kihali, yaliwasili Ijumapili kwenye wilaya ya Dungu, katika jimbo la Orientale, kaskazini-mashariki, katika JKK.

Taarifa ya takwimu za sasa kuhusu kipindupindu Zimbabwe

UM umeripoti takwimu za wagonjwa waliopatwa na kipindupindu katika Zimbabwe leo hii ni 23,712 na jumla ya vifo kwa sasa kutokana na maradhi ni 1,174.

Wataalamu wa Haki za Binadamu wahimiza mchango zaidi kudhibiti kipindupindu Zimbabwe

Wataalamu wanne wa UM juu ya haki za binadamu leo wametoa mwito maalumu wenye kuhimiza Serikali ya Zimbabwe pamoja na jumuiya ya kimataifa kuongeza mchango wao kwenye misaada ya kiutu kuwahudumia bora umma dhaifu na kukomesha janga liliotanda nchini la maradhi ya kipindupindu.

Mkutano wa Sirte ni wa daraja ya juu, asema mjumbe wa SADC

Kwenye mkutano mkuu wa siku tatu, wa kiwango cha mawaziri, uliofanyika kwenye mji wa Sirte, Libya wiki iliopita, kujadilia miradi ya kutunza maji kwa kilimo na kuzalishia nishati katika Afrika, kulikubaliwa rai ya kuchangisha mabilioni ya dola kukidhia mipangop hiyo ya maendeleo.