Ukuaji wa Kiuchumi

Ufufuaji wa utalii ni muhimu kwa uchumi Kenya, asema Mkuu wa UNEP

Achim Steiner, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) kabla ya kuondoka Nairobi Alkhamisi kuelekea Berlin, Ujerumani kunapofanyika maonyesho makubwa ya utalii duniani, aliwaambia wanahabari kwamba huduma za uchumi, pamoja na udhibiti bora wa viumbe anuwai, zinaweza kusawazishwa kwa natija za taifa zima, pindi utalii wa asili utafufuliwa tena nchini Kenya.

Hapa na pale

Bodi la Utawala la Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi wa Kimataifa (ILO) leo limeanza kikao chache cha 301, ambapo miongoni mwa masuala yatakayozingatiwa itajumuisha utekelezaji wa haki za kimsingi za ajira katika baadhi ya nchi, ushirikiano kati ya sekta za binafsi na kiraia, pamoja na kusailia shughuli za ILO za kuwasaidia wafanyakazi wahamiaji na udhibiti ubaguzi dhidi yao. ~

Juhudi za kupunguza umaskini Tanzania kwa kutumia nishati mbadala (Sehemu ya Pili)

Katika makala iliopita, tulikupatieni sehemu ya kwanza ya mazungumzo na Bariki Kaale, mtaalamu wa nishati katika ofisi ya Dar es Salaam ya Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Miradi ya Maendeleo Duniani (UNDP). Alisaiilia juhudi za wanavijiji kutumia kile alichokiita “nishati endelevu” iliyo rahisi, ambayo umma wa kawaida wataimudu na itawasaidia kukuza maendeleo yao kwa ujumla.

Mjumbe wa vijana asailia kikao cha CSD juu ya maendeleo

Neema Buhile, ni mwakilishi wa Vijana wa Nchi za Jumuiya ya Madola kutokea Tanzania ambaye hivi majuzi alikuwepo hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UM) kuhudhuria kikao cha mwaka cha Kamisheni juu ya Maendeleo ya Jamii (CSD). Muktadha wa mkutano huo wa mwaka ulilenga zaidi yale masuala yanayofungamana na ajira, ulemavu, hali ya kuzeeka na pia vijana. Redio ya UM ilipata fursa ya kuzungumza na Neema ambaye alitupatia maoni yake kuhusu ushirikiano unaofaa kuendelezwa na wajumbe wa kimataifa ili kuyatekeleza mapendekezo ya vikao vya kimataifa, kama kikao cha mwaka CSD, kwa mafanikio. ~~Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.

Fafanuzi za Mjumbe wa Tanzania juu ya kikao cha Kamisheni ya CSD

Naibu KM Asha-Rose Migiro alifungua rasmi kikao cha 46 Kamisheni ya CSD wiki iliopita ambapo alitilia mkazo kwenye hotuba yake juu ya “jukumu muhimu la ajira na kazi stahifu katika kukuza maendeleo”, hususan kwenye nchi zinazoendelea. Ernest Ndimbo, Mkurugenzi wa Ajira kwenye Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Watoto Tanzania alikuwa miongoni mwa wawakilishi waliohudhuria mkutano wa Kamisheni ya CSD. Ndimbo alifanya mahojiano maalumu na Redio ya UM ambapo alichukua fursa hiyo kutupatia fafanuzi zake kuhusu kikao cha mwaka huu cha Kamisheni ya CSD.~

Juhudi za kutumia nishati mbadala Tanzania kupunguza umasikini

Katika ziara niliyofanya Tanzania siku za nyuma, nilibahatika kuhudhuria warsha maalumu wa siku mbili katika Mkoa wa Kigoma, ambapo kulisailiwa taratibu za kukuza haraka maendeleo ya uchumi kwa kutumia nishati mbadala vijijini. Miongoni mwa mambo yaliyotatanisha wanawarsha ni kwamba utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hususan ile inayoambatana na matumizi ya nishati, huwa haulingani na ratiba ya mradi.

Mahojiano juu ya CSD na mjumbe wa Vijana wa Nchi za Jumuiya ya Madola

Neema Buhile, ni mwakilishi wa Vijana wa Nchi za Jumuiya ya Madola kutokea Tanzania ambaye yupo Makao Makuu akihudhuria kikao cha mwaka cha ile Kamisheni ya UM kuhusu Maendeleo ya Jamii (CSD). Muktadha wa kikao cha safari hii ulilenga zaidi kwenye masuala yanayofungamana na ajira, ulemavu, hali ya kuzeeka na pia vijana.

Uharibifu wa mazingira unachochea maangamizi ya mikoko duniani

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti kwamba baina ya miaka 1980 hadi 2005 asilimia 20 ya mikoko imeangamizwa duniani kutokana na uharibifu wa mazingira na pia kuzorota kwa uchumi, hasa katika nchi ziliopo Amerika ya Kati na Kaskazini na barani Afrika.

'Tuufanye 2008 kuwa mwaka wa kufyeka hali duni kwa mafukara bilioni' - Ban Ki-moon

KM wa UM Ban Ki-moon aliitisha kikao maalumu mwanzo wa 2008, kuzungumza na wanahabari wa kimataifa waliopo Makao Makuu mjini New York, ambapo alitathminia hali halisi juu ya kazi za UM. Kadhalika, alichukua fursa hiyo kutufafanulia mwelekeo anaopendelea uzingatiwe na jumuiya ya kimataifa katika kuimarisha kazi za UM, pamoja na kudhibiti bora miradi inayotekelezwa na mashirika yake kadha wa kadha katika sehemu mbalimbali za dunia. ~

'Tuufanye 2008 kuwa mwaka wa kufyeka hali duni kwa mafukara bilioni' - Ban Ki-moon

KM wa UM Ban Ki-moon aliitisha kikao maalumu mwanzo wa 2008, kuzungumza na wanahabari wa kimataifa waliopo Makao Makuu mjini New York, ambapo alitathminia hali halisi juu ya kazi za UM. Kadhalika, alichukua fursa hiyo kutufafanulia mwelekeo anaopendelea uzingatiwe na jumuiya ya kimataifa katika kuimarisha kazi za UM, pamoja na kudhibiti bora miradi inayotekelezwa na mashirika yake kadha wa kadha katika sehemu mbalimbali za dunia. ~