Ukuaji wa Kiuchumi

Mfanyakazi yuko njia panda : Afe kwa njaa au virusi? - ILO

Mikakati ya kutaka watu kubaki majumbani ili kuzuia kuenea kwa virusi vya ugonjwa wa Corona au COVID-19 imewaweka wafanyakazi njia panda akiwa hafahamu achague afe njaa na familia yake au afe kwa virusi.

COVID-19 inabadili mfumo wa usafirishaji haramu wa mihadarati :UNODC Ripoti

Ripoti mpya iliyotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu, UNODC imesema janga la virusi vya corona au COVID-19 limeathiri utaratibu wa usafirishaji haramu wa mihadarati hususan kwa njia ya anga na hivyo kuwafanya wasafirishaji haramu kusaka njia mbadala.

Tukiaadhimisha siku ya wafanyakazi duniani tuwakumbe wanaobeba mzigo wa COVID-19:Guterres

 Katika sehemu mbalimbali duniani leo ni sikukuu ya wafanyakazi, na mwaka huu kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku hiyo imeghubikwa na janga la virusi vya corona au COVID-19, na kwa hakika imedhihirisha kwamba kuna wafanyakazi ambao mara nyingi hubeba mzigo mkubwa bila kuonekana.

COVID-19 imeathiri wafanyakazi katika kila nyanja:ILO

Takwimu mpya zilizotolewa leo na shirika la kazi duniani ILO kuhusu athari za virusi vya corona au COVID-19 katika soko la ajira zinaonyesha kuna athari kubwa na mbaya kwa wafanyakazi wa sekta zisizorasmi za kiuchumi na kwa mamilioni ya makampuni duniani.

Je ni vipi biashara mtandaoni itakwamua nchi baada ya COVID-19?

Wiki ya biashara mtandao ya kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD ikianza hii leo, miongoni mwa mambo yanayoangaziwa ni jinsi ya kupata suluhu za kidijitali katika kusaidia dunia kujikwamua baada ya janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.

COVID-19 kuporomosha uchumi wa nchi za Afrika kusini mwa Sahara kwa asilimia 1.6- IMF

Shirika la fedha duniani, IMF limetaja mambo matatu muhimu ya kuzingatiwa ili kuweza kupunguza madhara ya kibinadamu na kiuchumi yatokanayo na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.
 

Uchumi wa dunia kuporomoka vibaya mwaka huu wa 2020-IMF

Mtazamo mpya uliotolewa na shirika la fedha duniani IMF kuhusu mwenendo wa uchumi duniani kwa mwaka huu 2020 unaonyesha kuwa ukuaji wa uchumi utakuwa katika hali hasi ya asilimia -3% kwa sababu ya mlipuko wa janga la virusi vya Corona au COVID-19.

Hata sisi wachora vibonzo, COVID-19 imeathiri kazi zetu-Nathan Mpangala

Ripoti ya hivi karibuni ilizotolewa na shirika la kazi duniani ILO ambayo inakubaliana na taarifa za shirika la fedha duniani IMF, inaonesha kuwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19, sekta ya ajira itaathirika kwa kiasi kikubwa na hivyo kuathiri uchumi wa dunia.

COVID-19 ina athari kubwa katika saa za kufanyakazi na mapato duniani:ILO

Mlipuko wa virusi vya Corona au COVID-19 umeelezwa kuwa na athari mbaya katika saa za kufanya kazi na mapato kote duniani kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na shirika la kazi duniani ILO ambaye inaainisha kanda na sekta zilizoathirika zaidi na kupendekeza sera za kukabiliana na mgogoro huu wa kimataifa.

Mradi wa UNDP Tanzania wabadili maisha ya wakazi wa Bunda mkoani Mara

Nchini Tanzania mradi wa mafunzo ya kilimo cha kisasa cha nyanya unaofadhiliwa na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, katika wilaya ya Bunda mkoani Mara umebadili maisha ya wakazi wa eneo hilo na hivyo kufanikisha lengo namba moja la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, la kutokomeza umaskini.