Utamaduni na Elimu

UM kusaidia wanasiasa Sierra Leone kupata welekevu wa vyombo vya habari

Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) pamoja na Ofisi ya Kufufua Kadhia za Uchumi na Jamii Sierra Leone (UNIOSIL) yamefanyisha warsha maalumu kwenye mji mkuu wa Freetown, Sierra Leone kuwasaidia wawakilishi wa vyama vya kisiasa kupatiwa uzoefu na welekevu juu ya mbinu za kuwasiliana na umma kwa kueneza ujumbe unaoambatana na itikadi zao za kisiasa, kwa kutumia vyombo vya habari.

Mila za Wenyeji wa Asili Kutunzwa kwa Teknolojia ya Kisasa ya Mawasiliano

Tume ya Kudumu ya UM kuhusu Haki za Wenyeji wa Asili ilikhitimisha mijadala yake ya mwaka mnamo tarehe 25 Mei (2007). Vikao ambavyo vilichukua wiki mbili vilijumuisha wawakilishi wa kutoka kanda mbalimbali za kimataifa, wakiwemo wajumbe wa kiserekali na mashirika yasio ya kiserekali, halkadhalika.

UNICEF yasaidia watoto 60,000 kupata vifaa vya maskuli

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetuma misaada ya vifaa vya skuli kwa wanafunzi watoto 60,000 waliopo kwenye yale maeneo sita ya Zambia yalioathiriwa na mafuriko yaliogharikisha sehemu hizo za nchi hivi karibuni.

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon aliwanasihi wajumbe wa kimataifa waliohudhuria Kikao cha Saba juu ua Demokrasia, Maendeleo na Biashara Huru, kilichofanyika Doha, Qatar kuhakikisha duru yao ya mazungumzo itawasilisha mafanikio ya kuridhisha, maana bila ya kuyafannya hayo, alionya, nchi masikini zitaporomoka zaidi kimaendeleo, hali ambayo anaamini itafumsha mitafaruku na kueneza hali ya wasiwasi kwenye mfumo mzima wa biashara katika soko la kimataifa.~

Haki halali za wenyeji wa asili, na athari za mabadiliko ya hali ya hewa

Baraza jipya la UM juu ya Haki za Binadamu lilipitisha, mnamo tarehe 29 Juni 2006, Azimio la Mwitiko wa Kuimarisha Haki za Wenyeji wa Asli Duniani. Azimio hili lilifanikiwa kupitishwa baada ya kufanyika kampeni ya miaka ishirini ziada, ambapo jumuiya zinazowakilisha jamii za wenyeji wa asili zilishirikiana na taasisi za Umoja wa Mataifa kadha wa kadha, na hatimaye, kuweza kuratibu mswada wa kuridhisha uliokuwa na makusudio ya kuwapatia wenyeji wa asili ulinzi wa kisheria na hifadhi bora ya haki za kimsingi, na za kijadi, halkadhalika. ~~

Mapitio juu ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Vijana katika UM

Wiki hii mamia ya vijana, kutokea Mataifa Wanachama 192 wa UM, walikusanyika kwa muda wa siku tatu katika Makao Makuu ya UM mjini New York na kujadiliana juu ya taratibu za kudhibiti mchango wao kwenye juhudi za kuyatekeleza Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

Juhudi za mtu mmoja kuwasaidia watoto wanaoishi na UKIMWI

Peter Mbiyu Kangethe, mjumbe wa baraza la serekali ya mitaa nchini Kenya ni moja ya raia wanaohusikana na juhudi za kupitisha sheria zitakazotumiwa kulinda maslahi ya yale watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI. ~

UNEP yafanyisha warsha wa kudhibiti mazingira Sudan.

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) wiki hii lilifanyisha warsha wa siku mbili mjini Khartoum, Sudan kuwapatia fursa wataalamu wahusika kubadilishana mawazo na fikra za kutunza na kuimarisha mazingira maumbile ya taifa,