Utamaduni na Elimu

Jamii ya kimataifa inahimizwa na KM kuimarisha ari ya Olimpiki

KM wa UM Ban Ki-moon amewasilisha risala maalumu, kwa kupitia njia ya vidio kuhusu Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu itakayofanyika Beijing, Uchina. Risala imependekeza vita isitishwe kote duniani katika kipindi chote michezo ya Olimpiki inafanyika Uchina, kuanzia mwezi Agosti. Kwa mujibu wa risala ya KM, malengo ya maadili ya kimsingi ya Michezo ya Olimpiki hufanana sawa na yale ya UM: hasa katika kukuza mafahamiano na kuhishimiana kati ya wanadamu; na katika majukumu ya kuandalia umma wa kimataifa fursa ya kufanikiwa, kwa usawa, kimaendeleo kwa kufuata taratibu na sheria; na muhimu ya yote katika kuimarisha utulivu na amani kwa wote.

Hapa na pale

Warsha maalumu pamoja na tafrija mbalimbali zinafanyika Makao Makuu ya UM kuadhimisha miaka 10 tangu Sheria ya Roma ilipoidhinishwa na kuanzishwa Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC). KM Ban Ki-moon alisema kuanzishwa kwa Mahakama ya ICC ni moja ya mafanikio makubwa ya karne iliopita.~

CITES inakutana Geneva kusailia biashara ya pembe na mbao adimu

Mkutano wa UM wa kikao cha 57 cha Kamati Ndogo juu ya utekelezaji wa Mkataba wa Biashara ya Kimataifa kuhusu Udhibiti wa Aina za Wanyama na Mimea Pori Inayohatarishwa Kuangamia (CITES) unafanyika Geneva wiki hii, kuanzia tarehe 14 Julai hadi 18 kuzingatai ombi la Uchina kuruhusiwa kuagizishia tani 100 za pembe za ndovu kutoka Afrika, akiba ambayo imevumbikwa sasa hivi kwenye maghala ya nchi nne za Kusini ya Afrika.

Maeneo manane mapya kuingizwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO

Kamati ya Shirika la UM juu ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayokutana hivi sasa kwenye Mji wa Quebec, Kanada kuzingatia mirathi ya walimwengu, imeafikiana kuingiza maeneo kadha mapya ziada ya kihistoria kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia.

Kamati ya Mirathi ya Kimataifa yazingatia maeneo mapya ya urithi wa umma

Kamati inayohusika na Orodha ya UNESCO juu ya Mirathi ya Dunia inakutana kwenye mji wa Quebec, Kanada kuanzia tareha 02 mpaka 10 Julai kuzingatia maeneo mapya ya kimataifa yanayohitajika kutambuliwa na kuingizwa kwenye Orodha ya Mirathi ya Umma wa Ulimwengu.

Ripoti juu ya juhudi za kufufua nafasi za elimu mitaani Kenya

Wiki hii tuna ripoti kuhusu juhudi za kufufua huduma za elimu ya msingi katika Kenya, ambazo ziliharibiwa na machafuko yaliotukia nchini humo kufuatia uchaguzi wa mwisho wa 2007.~

WaMaasai wa Kenya watasaidiwa na UM kutunza utamaduni wa jadi

Shirika la UM juu ya Hakimiliki za Kitaaluma (WIPO) limeripoti kwamba raia wawili wa KiMaasai wa Laikipia, Kenya wamepatiwa fursa ya kwenda Marekani kushiriki kwenye mafunzo maalumu ya Taasisi ya Kuhifadhi Utamaduni wa Kienyeji, mafunzo ambayo yanatarajiwa kuwapatia ujuzi wa kisasa wa kutunza na kuhifadhi nyaraka za utamaduni wao wa jadi, kwa masilahi ya vizazi vijavyo. ~~

Papa Benedict XVI azuru Makao Makuu ya UM

Papa Benedict XVI leo asubuhi alizuru Makao Makuu ya UM ambapo alikutana na KM Ban Ki-moon pamoja, Raisi wa Baraza Kuu Srgjan Kerim na vile vile wafanyakazi wa UM waliopo mjini New York.

Mataifa yenye watu wingi duniani yanazingatia elimu ya msingi kwa wote

Mawaziri na wataalamu wa elimu kutoka nchi tisa zenye kujumuisha nusu ya umma wa ulimwengu, yakiwemo Bangladesh, Brazil, Uchina, Misri, Bara Hindi, Mexico, Nigeria na pia Pakistan yanakutana wiki hii Bali, Indonesia chini ya uongozi wa Shirika la UM juu ya Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupanga miradi itakayoyawezesha kuharakisha lengo la kuwapatia watoto wote elimu ya msingi kwenye maeneo yao.

Usomali kupwelewa kuandikisha watoto wa skuli za msingi, imeonya UNICEF

Veronique Taveau, Msemaji wa UNICEF mjini Geneva aliwaambia waandishi habari Ijumaa kwamba taifa la Usomali lina sifa mbaya ya uandikishaji mdogo kabisa wa watoto wanaohudhuria skuli za msingi, hususan watoto wa kike. Hivi sasa imebainishwa kwamba idadi ya watoto wa kike wanaohudhuria skuli za msingi nchini ni 121,000. UNICEF impenedekeza idadi hiyo iongozwe mara mbili katika 2009 na wanalenga kuwapatia watoto wa kike 50,000 fursa ya kuhudhuria skuli za msingi mwakani.~~