Utamaduni na Elimu

UNICEF inasaidia kupambana na Ukimwi DR Congo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumiwa watoto UNICEF nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limekuwa likianisha kazi za ofisi yake katika mji wa Lubumbashi ambayo ni kupambana ukosefu wa uelewa wa kutosha miongoni mwa watu wa kuzuia virusi vya HIV na ukimwi.

UNESCO imezindua mchezo kwenye wavuti kuelimisha vijana kuhusu Ukimwi

Umoja wa Mataifa umezindua mchezo wa video kwa kutumia wavuti kwa lengo la kuwapa vijana taarifa muhimu kuhusu kuzuia maambukizi ya HIV, huku ukiwaelimisha, kuwaburudisha na kuchagiza tabia njema zinazojali afya zao.

Leo ni siku ya Kimataifa ya Mshikamano kwa watu

Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa watu inaainisha umuhimu wa kuchukua hatua ya pamoja kwa maslahi ya watu wasiojiweza katika jamii amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon.

Akiutazama mwaka 2010 Ban amesema umekuwa wa kishindo kwa UM

Katika mkutano wake wa mwisho wa mwaka na waandishi wa habari hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema 2010 umekuwa mwaka wa kishindo kwa Umoja wa Mataifa.

Usanii unachangia kukua kwa uchumi:UNCTAD

Biashara inayohusika na usanii imetajwa kuwa moja ya vitu vinavyochangia kuimarika kwa uchumi.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD.

Mshauri wa UM kuhusu michezo ahofia kufungwa kwa NGO ya vijana Gaza

Mshauri maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu michezo kwa maendeleo na amani bwana Wilfried Lamke amelezea hofu yake kuhusu kufungwa kwa nguvu ofisi zote za Sharek Youth Forum ambazo sio za kiserikali zinazohusika na masuala ya vijana.

Mwaka wa kimataifa wa watu wenye asili ya Kiafrika wazinduliwa

Mwaka wa kimataifa wa watu wenye asili ya Kiafrika umezinduliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.

Siku ya milima duniani kuadhimishwa juma hili

Siku ya milima duniani ya kila mwaka inaadhimishwa tarehe 11 mwezi huu.

WHO kutoa mpangilio wa viwango vya madawa ya kienyeji

Shirika la afya duniani WHO linatarajiwa kuanzisha mpango wa kwanza kabisa ya kuyatambua madawa ya kienyeji na kutambua manufaa yake.

Bila kuwakwamua walemavu hatuwezi kutokomeza umasikini:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitolea wito serikali zote kuongeza juhudi kuwasaidia walemavu kwani amesema bila kutatua matatizo yao , vita dhidi ya umasikini, maradhi na maendeleo duni hatuwezi kuvishinda.