Utamaduni na Elimu

UNICEF inasema, usalama wa watoto maskulini wategemea majengo madhubuti

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) leo limetoa mwito maalumu wenye kuhimiza kuchukuliwa juhudi za pamoja, na za lazima, na jumuiya ya kimataifa, kwa makusudio ya kuimarisha majengo ya skuli ili kuhakikisha yanakuwa salama kwa watoto.

Twamkumbuka Mama Afrika - Miriam Makeba

Tarehe 27 Novemba 2008 ni Siku Kuu ya Kutoa Shukrani nchini Marekani, na kawaida ofisi zote hufungwa, ikijumuisha vile vile ofisi za Makao Makuu ya UM, ziliopo jiji la New York, Marekani. Hata hivyo, Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM imewajibika kutayarisha vipindi katika siku hii. Ilivyokuwa hii ni Siku Kuu ya Kutoa Shukrani, nasi pia tumeamua kuandaa makala maalumu, yenye kuwasilisha shukrani za jumuiya ya kimataifa, kwa ujumla, kuhusu mchango wa Balozi Mfadhili wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO), Mama wa Afrika, msanii maarufu wa Afrika Kusini, marehemu Miriam Makeba katika kuhudumia kihali umma uliokabiliwa na matatizo ya ufukara na hali duni.~

Utovu wa elimu sawa duniani hutomeza mamilioni ya watoto kwenye hali duni, inasema ripoti ya UNESCO

Shirika la UM juu ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetoa ripoti maalumu leo yenye kuonyesha ya kuwa tofauti za fursa katika elimu ni kadhia ambayo hukandamiza mamilioni ya watoto wanaomalizikia kwenye maisha ya umaskini na ambao hunyimwa fursa za kujiendeleza kimaisha.

Matumizi ya dini kuhalalisha ugaidi, na mauaji ya wasiodhuru, yapingwa kidhati na kikao maalumu cha BK

Mkutano wa siku mbili wa Baraza Kuu, uliohudhuriwa na wawakilishi wote, kuzingatia juhudi za kuimarisha “Utamaduni wa Amani” ili kukomesha hali duni na mitafaruku duniani na kukuza maelewano na mafahamiano miongoni mwa nchi wanachama, kikao hicho kilihitimishwa Alkhamisi usiku ambapo wajumbe wa kimataifa waliafikiana kupinga matumizi ya dini kuhalalisha vitendo vya mauaji ya watu wasio hatia, na pia kulaani vitendo vya kigaidi.

Majadiliano ya imani anuwai yahimizwa na BK kuimarisha amani duniani

Baraza Kuu la UM linaendelea na siku ya pili ya mkutano unaohudhuriwa na wawakilishi wote ambapo wajumbe wa kimataifa walibadilishana mawazo na kujadiliana maoni kuhusu utaratibu wa kutekelezwa kipamoja kuimarisha “Utamaduni wa Amani” ulimwenguni.

Baraza Kuu linasailia utamaduni wa amani

Baraza Kuu la UM leo limeanzisha majadiliano ya jumla, ya siku mbili, kwenye kikao cha wawakilishi wote, kuzingatia namna dini mbalimbali zitatumia kile kilichotafsiriwa kama “Utamaduni wa Amani” kusaidia umma wa kimataifa kutatua, kipamoja, yale masuala yanayodhalilisha ubinadamu, mathalan, umaskini na njaa.

Siku ya Kimataifa kuhishimu watu wa umri mkubwa

Tarehe 01 Oktoba huadhimishwa na UM kama ni Siku Kuu ya Watu Wenye Umri Mkubwa. Siku hii hutumiwa na jamii ya kimataifa kukumbushana umuhimu na ulazima wa kuupatia umma wa watu wakongwe hali njema ya afya, raha, ustawi na hishima, mambo ambayo yameonekana kukosekana katika miaka ya karibuni, licha ya kuwa Mataifa Wanachama yalishaahidi kuondosha ubaguzi dhidi ya fungu hili kubwa, na muhimu, katika jamii zao, umma ambao kila siku hunyimwa haki halali za kimsingi.~~

UM unaadhimisha Siku ya Kujizuia Kujiua Duniani

Mnamo tarehe 10 Septemba kila mwaka UM huiadhimisha siku hiyo kuwa ni Siku ya Kuzuia Kujiua Duniani. Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zimeonyesha, kwa wastani, watu 3000 huamua kujiua kila siku duniani kwa sababu ya mawazo, fikra na mambo kadha wa kadha yanayomkumba mwanadamu.

UM inaadhimisha Siku ya Kimataifa juu ya Ujuzi wa Kusoma na Kuandika

Tarehe 08 Septemba inaadhimishwa kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Ujuzi wa Kusoma na Kuandika. Mada ya taadhima ya mwaka huu imetilia mkazo fungamano ziliopo kati ya uwezo wa mtu kusoma na kuandika na afya bora.

BK linamkumbuka raisi wa Zambia/kusailia azimio la ugaidi duniani

Baraza Kuu (BK) la UM asubuhi limekutana kujadilia azimio linalohusu mbinu za kupiga vita ugaidi duniani, kikao ambacho kilihudhuriwa na Raisi wa Baraza Kuu, KM na wawakilishi kadha wa kadha wanachama.