Tabianchi na mazingira

Nchi masikni zataka nchi tajiri zitimize ahadi zao za kuwapatia fedha

Mafuriko makubwa, mioto ya nyika inayoangamiza misitu, na kupanda kwa kina cha bahari pamoja na maelfu ya maisha ya watu yanayokatizwa na majanga hayo  na riziki wza watu zinazoendelea kuathiriwa, ni hali halisi ambayo mataifa mengi tayari yanakabiliana nayo.  

Fedha ndio mtihani mkubwa kwa nchi kukabiliana na afya na mabadiliko ya tabianchi:WHO

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO leo limesema nchi nyingi zimeanza kuweka kipaumbele cha afya katika juhudi zao za kuwalinda watu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi, lakini ni takriban robo tu ya wale waliofanyiwa utafiti hivi karibuni na Shirika hilo wameweza kutekeleza kikamilifu mipango au mikakati yao ya kitaifa ya afya na mabadiliko ya tabianchi.

COP26: Watu wa asili wana nafasi kubwa ya pekee katika kuzuia mabadiliko ya tabianchi 

Mamilioni ya watu wameingia kwenye mitaa ya miji kote ulimwenguni ikiwa ni pamoja na viunga vya mji wa Glasgow nchini Uskochi unakofanyika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi COP26 wakidai hatua kubwa zaidi ya tabianchi huku nchi zinazoshiriki katika mazungumzo ya COP26 zikiwa zimeahidi kuwekeza katika masuluhisho yasiyoharibu tabianchi kupitia kilimo.  

Vijana washika hatamu COP26 wakitaka vitendo kulinda tabianchi

“Tunataka nini? Haki kwa tabianchi! Tunataka lini? Sasa!” Kauli hizo zimesikika zikipazwa na vijana eneo lote la kati la mji wa Glasgow huko Scotland hii leo Ijumaa wakati maelfu ya waandamanaji walipoingia mitaa ya mji katika siku ambayo mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26 ulitenga kwa ajili ya vijana

Nusu ya watu duniani watakuwa katika hatari ya mafuriko, vimbunga na Tsunami ifikapo 2030:UN

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu Tsunami Umoja wa Mataifa umeonya kwamba kufikia mwaka wa 2030, inakadiriwa kuwa asilimia 50 ya watu wote duniani wataishi katika maeneo ya pwani ambayo yanakabiliwa na mafuriko, vimbunga na tsunami. 

Vijana tunaweza ni wakati wa kutushirikisha kwa vitendo katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:Nzambi

Wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP26 ukiendelea mjini Glasgow Scotland, vijana wanatoa wito kwa viongozi kutekeleza kwa vitendo ushirikishwaji wa vijana katika vita dhidi ya janga hilo.

Siku ya nishati COP26 yasikia vilio vya kutaka makaa ya mawe yasalie historia

Katika siku ya nne ya mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26 huko Glasgow, Scotland, sauti zimepazwa na wanaharakati wakitaka kukomeshwa kwa matumizi ya makaa ya mawe nishati ya gesi na mafuta, sauti ambazo zimepaswa siku ambayo mkutano huo ulikuwa unamulika nishati.

COP26: Hakuna tena maneno matupu, sekta binafsi zajitoa kimasomaso- Carney

Katika siku inayomulika sekta ya fedha na udhibiti wa mabadiliko ya tabianchi kwenye mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mabadiliko ya tabianchi, COP26 huko Glasgow, Scotland, takribani kampuni binafsi 500 zimekubaliana kutenga dola trilioni 130 kutekeleza mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi ikiwemo hakikisha kiwango cha joto duniani hakizidi nyuzijoto 1.5  katika kipimdo cha Selsiyasi. 

Lazima kuwe na uwajibikaji katika ukiukwaji mkubwa wa haki Tigray:OHCHR Ripoti

Utafiti wa Pamoja uliofanywa na tume ya haki za binadamu nchini Ethiopia (EHRC) na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) umebaini kwamba kuna sababu za msingi za kuamini kwamba pande zote katika mzozo wa Tigray nchini Ethiopia kwa kiasi fulani wamekiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu, sheria za ubinadamu na sheria za wakimbizi, ukiukwaji ambao unaweza kuwa ni uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Zaidi ya nchi 100 zimeahidi kusitisha na kubadilisha ukataji miti ifikapo 2030

Azimio la kihistoria la kuokoa na kurejesha misitu ya dunia katika ubora wake limetangazwa leo rasmi katika siku ya pili ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi unaoshirikisha viongozi wa dunia au COP26.