Hatimaye dau la plastiki lililosafiri kilometa 500 kutoka Lamu, nchini Kenya hadi Mji Mkongwe, Zanzibar nchini Tanzania limetia nanga Unguja likiwa limetimiza azma yake ya kuelimisha jamii zilipo pwani kwa Kenya na Tanzania kuhusu madhara ya plastiki kwa binadamu, mazingira na viumbe vya majini.