Tabianchi na mazingira

Mkutano wa WCC unazingatia utaratibu mpya wa kueneza taarifa za hali ya hewa kote duniani

Mkutano Mkuu wa Dunia juu ya Hali ya Hewa (WCC-3) umefunguliwa rasmi Geneva Ijumatatu ya leo, ambapo wataalamu na wanasiasa kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu, wanakutana kwa mashauriano ya kuhakikisha umma wa kimataifa huwa unapatiwa uwezo wa kutabiri hali ya hewa pamoja na taarifa nyengine kama hizo, ili kukabiliana vyema na taathira za mabadiliko ya hali ya hewa.

Siku 100 zimesalia kabla ya Mkutano wa COP-15 kudhibiti taathira za mabadiliko ya hali ya hewa

UM umetoa mwito maalumu wenye kuwataka mamilioni ya umma wa kimataifa kutia sahihi zao, kwenye mtandao, ili kuidhinisha lile ombi la kuzihimiza serikali wanachama Kukamilisha Makubaliano juu ya waraka wa Mkutano wa COP-15, yaani ule Mkutano Mkuu utakaofanyika mwezi Disemba katika mji wa Copenhagen, Denmark kuzingatia mkataba mpya wa udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

Mabadiliko ya hali ya hewa yabatilisha historia kuwa ni kiashirio kwa wakulima, anasema Mkuu wa WMO

Michel Jarraud, Mkuu wa Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) amenakiliwa akisema mabadiliko ya hali ya hewa yameifanya tarikh/historia kuwa ni chombo kisio sahihi tena katika kuongoza shughuli za wakulima, pamoja na wale wawekezaji wa kwenye nishati.

Wataalamu wa mkataba wa kudhibiti silaha za kibayolojia wanakutana Geneva

Wataalamu magwiji wa fani ya silaha zinazotumia vijidudu vya viumbehai wanakutana hivi sasa mjini Geneva kusaillia maendeleo katika ujenzi wa fani ya uchunguzi wa maradhi ya vijidudu hivyo, ugunduzi wake, utambuzi wa ugonjwa na udhibiti wake.

Vijana wawasihi viongozi wa dunia kuonyesha vitendo kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Vijana na Watoto wa Kimataifa wa TUNZA, uliofanyika kwenye mji wa Daejeon, Korea ya Kusini walipokamilisha vikao vyao mwisho wa wiki iliopita walitoa mwito maalumu unaowataka viongozi wa dunia kuchukua hatua kali, za dharura, kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ulimwenguni.

Mkutano wa Stockholm wasisitiza ulazima wa kujumuisha suala la maji kwenye kikao cha COP-15

Wajumbe walioshiriki kwenye mkutato unaoadhimisha Wiki ya Maji Duniani kwa 2009, unaofanyika kwenye mji wa Stockholm, Sweden wamepitisha hii leo kwa kauli moja azimio linalosema suala la maji ni laizma kujumlishwa kwenye kikao cha COP-15,

Hapa na Pale

KM Ijumanne amemaliza ziara yake katika Jamhuri ya Korea/Korea ya Kusini. Kabla ya kuondoka mji mkuu wa Seoul, KM alizuru madhabahu ya kuomboleza yaliopo hospitali, kumhishimu aliyekuwa Raisi wa Jamhuri ya Korea, Kim Dae-jung, ambaye alifariki siku ya leo.

Maendeleo machache yalipatikana kwenye kikao cha Bonn, asema Mkuu wa UNFCCC

Mkutano wa wiki moja kuzingatia vifungu vya waraka wa kujadiliwa kwenye Mkutano wa Copenhagen kuhusu udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa, utakaofanyika mwezi Disemba, Ijumaa ya leo, umekamilisha mashauriano yake mjini Bonn, Ujerumani. Wajumbe wa kimataifa 2400 walihudhuria kikao hicho cha Bonn.

Mazungumzo ya kudhibiti marekebisho ya hali ya hewa yameanzisha duru nyengine Bonn

Hii leo kwenye mji wa Bonn, Ujerumani wajumbe wa kimataifa wamekusanyika tena kwenye duru nyengine ya kikao kisio rasmi, kushauriana juu ya maafikiano yanayotakikana kukamilishwa kwenye Mkutano Mkuu ujao, wa kupunguza umwagaji wa hewa chafu ulimwenguni, utakaofanyika mwezi Disemba mjini Copenhagen, Dennmark.

Shambulio la awali la atomiki Hiroshima lakumbukwa na Mkutano wa Kuondosha Silaha Duniani

Tarehe ya leo, Agosti 06, 2009 ni siku ya ukumbusho wa kutupwa kwa bomu la kwanza la atomiki, na vikosi vya anga vya Marekani, katika mji wa Hiroshima, Ujapani miaka sitini na nne iliopita.