Tabianchi na mazingira

Baada ya kuzuru Asia KM awaonya walimwengu juu ya hatari ya taathira za mabadiliko ya hali ya hewa

Ijumatano, tarehe 29 Julai 2009, KM Ban Ki-moon alikuwa na mazungumzo na waandishi habari wa kimataifa waliopoMakao Makuu kuzingatia safari ya wiki moja aliyoyatembelea mataifa mawili ya Asia, yaani Uchina na Mongolia.

Ban anasema ni muhimu kwa Mataifa kuhitimisha mashauriano ya mkataba wa kudhibiti hali ya hewa

KM Ban Ki-moon leo alikuwa na mazungumzo ya kila mwezi na waandishi habari wa kimataifa waliopo hapa Makao Makuu ya UM. Kwenye taarifa ya ufunguzi KM alizingatia zaidi suala la athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni na juhudi za kimataifa za kulidhibiti tatizo hili.

Mashirika ya kimataifa yameandaa mradi wa kutoa hadhari za mapema dhidi ya miripuko ya moto

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) likijumuika na Shirika la Ulaya juu ya Anga Nje ya Dunia (ESA), pamoja na Shirika la Marekani Linalosimamia Uchunguzi wa Anga (NASA) yameripoti juu ya umuhimu wa kudhibiti haraka miripuko ya moto ilioshuhudiwa kutukia ulimwenguni katika siku za karibuni, kwenye sehemu mbalimbali za dunia, hasa yale maeneo ya karibu na Bahari ya Mediterranean, kusini ya Jangwa la Sahara, Australia na katika Amerika ya Kaskazini.

Ban ausihi ulimwengu ujirekibishe kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

KM Ban Ki-moon, kwenye hotuba alioitoa Ulaanbaatar, mji mkuu wa Mongolia Ijumatatu ya leo, kuhusu "Marekibisho ya Kudhibiti Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani" alieleza kwamba nchi zilizozungukwa na bara husumbuliwa sana na vizingiti vinavyokwamisha juhudi za kusukuma mbele maendeleo yao, hususan katika kipindi ambacho nchi hizi zisio na pwani huwa zinaathirika pia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa,

Ban anaamini miradi ya kudhibiti uchafuzi wa hali ya hewa Uchina inaweza kurudiwa kimataifa

KM Ban Ki-moon, ambaye anafanya ziara ya siku nne katika Uchina, Ijumaa alihudhuria mjini Beijing, tukio la kuanzisha mradi bia wa UM na Serikali ya Uchina kuhimiza umma wa huko, kutumia ile balbu ya taa yenye kuhifadhi nishati na inayotumika kwa muda mrefu.

Mafanikio ya Mkutano wa Copenhagen yatahitajia $10 bilioni, anasema de Boer

Yvo de Boer, Katibu Mtendaji anayesimamia Mfumo wa Mkataba wa Kimataifa Kudhibiti Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani, amenakiliwa akisema kunahitajika mchango wa dola bilioni 10 kudhibiti, kihakika, athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

Walinzi amani wa UM katika Liberia wameanzisha mazoezi mapya kutunza mazingira

Vikosi vya ulinzi amani vya UM viliopo katika jimbo la Kakata, Liberia Magharibi vimeanzisha mazoezi mapya mnamo mwanzo wa mwezi huu, yaliokusudiwa kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

Hapa na pale

Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jana lilimaliza Mkutano wa Dunia juu ya Iimu ya Juu uliofanyika Paris, ambapo kulitolewa mwito maalumu unaozitaka nchi wanachama kuongeza mchango wao katika juhudi za kukuza ilimu. Kwenye taarifa rasmi ya mkutano, wajumbe waliowakilisha nchi 150 walitilia mkazo umuhimu wa kuwekeza posho ya bajeti lao kwenye sekta ya ilimu, ili kujenga jamii yenye maarifa anuwai, na inayomhusisha kila raia, ambaye atapatiwa fursa sawa ya kushiriki kwenye tafiti za hali ya juu, huduma itakayowakilisha uvumbuzi na ubunifu wenye natija kwa umma.

KM amehadharisha viongozi wa G-8 kwamba uamuzi wao wa kupunguza hewa chafu hauridhishi

KM Ban Ki-moon Alkhamisi ya leo alihutubia kikao maalumu, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Viongozi wa Mataifa Yenye Uchumi Mkuu wa Kundi la G-8, unaofanyika kwenye mji wa L\'Aquila, Utaliana.