Tabianchi na mazingira

Siku ya Kimataifa Kuhishimu Viumbe Hai Anuwai

Tarehe ya leo, 22 Mei (2009) ni mwezi unaodhamishwa kila mwaka na UM kama ni Siku Kuu ya Kimataifa ya Kuhishimu Viumbe Hai Anuwai.

UNFCCC imeripoti maendeleo kwenye majadiliano kuhusu udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa duniani

Taasisi ya UM ya juu ya Utendaji wa Mkataba wa Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani (UNFCCC) imetoa ripoti rasmi, ya kurasa 53, yenye mapendekezo kadha wa kadha, ya kuzingatiwa na kutekelezwa na mataifa yote wanachama, ikijumlisha mataifa tajiri na maskini, ili kudhibiti bora taathira haribifu zinazochochewa na hali ya hewa isio ya kikawaida wakati nchi wanachama zitakapokutana Copenhagen, baada ya siku 200 zijazo.

Wanakijiji wa Kenya wadhaminiwa mradi wa kudhibiti kaboni kwa natija za mazingira

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limeripoti kuanzishwa mradi wa maendeleo wa kuwashirikisha wanavijiji kutoka Kenya magharibi ili kutunza vyema mazingira yao.

FAO/UNEP yahadharisha dhidi ya athari haribifu kutoka 'uvuvi wa mapepo' baharini

Taarifa mpya, iliotolewa kwa pamoja baina ya Shirika a UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) na Shirika la Hifadhi ya Mazingira (UNEP) imehadharisha juu ya kuselelea kwa hatari ya kimazingira na biashara, inayochochewa na vifaa vya uvuvi vilivyopotea au kutupwa baharini kihorera na wavuvi, vitu ambavyo vimethibitika huharibu sana maumbile ya baharini, na kuathiri bidhaa ya samaki kwa sababu ya uvuvi unaojulikana kama "uvuvi wa kizimwi na mapepo".

Mfumo wa tahadhari ya mapema maafa unafanyiwa mapitio na wataalamu wa WMO

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limeripoti wataalamu 90 kutoka nchi wanachama walikutana kwenye Makao Makuu ya Geneva, kutathminia ubora wa hewa na mabadiliko ya hali ya hewa yaluiojiri ulimwenguni pamoja na athari zake.