Msimu wa upanzi ukianza nchini Ethiopia, serikali nayo inahaha kudhibiti kuenea kwa nzige wavamizi wa jangwani huku wakulima nao wakilalama vile ambavyo wadudu hao waharibifu wanaleta hofu na shaka kubwa hivi sasa.
Wito wa Umoja wa Mataifa wa kutaka wahisani kusaidia harakati za kukabiliana na nzige wavamizi wa jangwani huko Mashariki mwa Afrika umeanza kuitikiwa ambapo msaada wa karibuni zaidi ni wa dola milioni 10 kutoka taasisi ya Bill na Melinda Gates.
Mvua kubwa zilizonyesha kwa wiki mbili zilizopita nchini Madagascar zimeathiri watu 120,000 ikiwakata kabisa na huduma za barabara, kusambaratisha shule 174, na kuwalazimisha watu 16,000 kusalia bila makazi.
Hofu mpya ya athari za mabadiliko ya tabianchi katika sayari dunia imechochewa na thibitisho la shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kwamba Antarctic imeshuhudia viwango vya rekodi mpya ya joto Kali ambalo limepindukia zaidi ya nyuzi 18C .