Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA , idadi ya vifo vilivivyosababishwa na athari za kimbunga Idai nchini Msumbiji imeongezeka na kufikia 493.
Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema linajiandaa kuzisaidia jamii za vijijini zilizoathirika na kimbunga IDAI nchini Msumbiji kufufua kilimo na masuala ya uvuvi.
Dalili za wazi na athari za kiuchumi na kijamii zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi zinazongezeka kote duniani kukishuhudiwa kiwango kikubwa cha hewa chafuzi ya viwandani inayosababisha ongezeko la joto na kufikia viwango vya hatari, kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO.
Hali tete inaendelea katika sehemu kubwa ya Kusini mwa afrika iliyoathirika na kimbunga IDAI kwani mvua kubwa zinaendelkea kunyesha na kusababisha uharibifu mkuwa sababu ya mafuriko umesema leo Umoja wa Mataifa , huku timu za misaada ya kibinadamiu zikifanya kila liwezekanalo kunusuru maisha ya watu na kuwafikia wanaohitaji zaidi msaada.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema anatambua shaka na shuku walizo nazo vijana kuhusu mustakabali wa mazingira lakini bado ana matumaini kwa siku za usoni.
Mkutano wa nne wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa ukiendelea huko Nairobi, Kenya, Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo Amina J. Mohammed ametaka mwaka huu wa 2019 uwe mwaka wa kuibuka na suluhu zenye mabadiliko dhidi ya uharibifu wa mazingira.
Uharibifu wa sayari dunia ni mkubwa sana na afya za wakazi wa dunia hiyo zipo hatarini iwapo hatua hazitachukuliwa hivi sasa, imesema ripoti ya hali ya mazingira iliyotolewa hii leo na shrika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP.
Kwa mara nyingine Malawi imekumwa na mafuriko makubwa yaliyokatili maisha ya watu, kusababisha uharibifu mkubwa na kuwafungisha virago mamia ya watu ambao sasa wanahitaji msaada umesema Umoja wa Mataifa.
Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP linasambaza msaada wa dharura wa chakula kwa watu 134,000 waliokumbwa na uhaba wa chakula kutokana na mabadiliko ya tabianchi huko jimbo ni Kirundi nchini Burundi.