Wakati amani ya Yemen ikiwa katika hali mbaya na pia kukiwa na uhaba wa chakula, Muungano wa Ulaya na shirika la chakula na kilimo duniani FAO leo mjini Amman, Jordan, wametangaza mchango mpya uliotolewa na muungano wa ulaya wa kiasi cha dola milioni 6.7 dola katika kuunga mkono kazi ya FAO ya kujenga uwezo wa Yemen kushughulikia masuala yanayosababisha uhaba wa chakula.