Wakati mamia ya watunga sera wakikusanyika huko Marrakech nchini Morocco kwa ajili ya kukubaliana juu ya mkataba mpya wa kimataifa kuhusu uhamiaji, mkutano wa 24 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP24 huko Katowice Poland, nao unajikita katika njia thabiti za kusaidia nchi kukabiliana na ukimbizi wa ndani utokanao na madhara ya mabadiliko ya tabianchi ikiwemo ukosefu wa maji, mafuriko, vimbunga na kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari