Sisi ni kizazi cha kutokomeza njaaTunaweza kuwa kizazi cha kwanza kufanikiwa kutokomeza njaa, kama ambavyo tunaweza kuwa kizazi cha mwisho kuikoa dunia.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza masikitiko yake makubwa kufuatia ripoti za vifo vya watu vilivyosababishwa na kimbunga Mangkhut nchini Ufilipino.
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuhifadhi tabaka la ozoni, Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema mwaka huu umevunja rekodi ya joto kali duniani kote na pia kuwa ni wakati muhimu kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Katibu Mtendaji wa mkataba wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa wa tofauti za kibiolojia, Dkt. Cristiana Paşca Palmer amezungumzia umuhimu wa mkutano wa kimataifa kuhusu bayonuai utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu huko Sharm el-Sheikh nchini Misri.
Mwishoni mwa waka huu wa 2018 kuna uwezekano mkubwa wa kuzuka matukio ya El Nino kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo na shirika la hali ya hewa duniani WMO.
Mataifa 24 likiwemo moja linalopakana na baharí ya Hindi yanashiriki kuanzia leo Jumanne katika zoezi la” wimbi la baharí ya Hindi 2018, au IOwave 2018,” litakalojikita katika hali mbili.