Tabianchi na mazingira

Watoto wamekuwa wahanga wakubwa wa mabadiliko ya hali ya hewa duniani:UNICEF

Matukio mengi ya hali mbaya ya hewa duniani yakiwemo mafuriko kusini mwa India, moto nyikani huko magharibi mwa Marekani na joto la kupindukia katika eneo la kaskazini mwa dunia, yanawaweka watoto katika hatari na kutishia hatima yao, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,  UNICEF imeonya hii leo.

Ukame waongeza machungu kwa wananchi Afghanistan

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema mzozo unaoendelea nchini Afghanistan, majanga ya asili, ukimbizi wa ndani vinaendelea kusababisha ongezeko la ukosefu wa uhakika wa chakula nchini humo.

Sudan Kusini yaweka vikwazo vya kuuza mkaa nje ya nchi

Serikali ya Sudan Kusini imetangaza udhibiti wa uuzaji wa mkaa nje ya nchi hiyo kuanzia mwezi uliopita wa Julai. Hatua hiyo iliyotangazwa na Waziri wa Biashara wa Sudan Kusini Dkt. Moses Hassan Tiel imetaka maafisa wote wa biashara nchini humo walioko katika vituo vya mipakani pamoja na vyombo vya usalama, vya kuzuia biashara ya magendo na mashushu wa masuala ya kiuchumi kuhakikisha udhibiti huo unatekelezwa nchini kote.

 

Kisiwa cha marashi kiko hatarini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi:UNDP

Comoro, ni kisiwa kimesheheni fukwe mwanana, milima ya volkano, manukato ya maua ya ylang-ylang yanayotoa mafuta ya uzuri, lavani au vanila na karafuu, ni kisiwa kilichoko kwenye baharí ya Hindi katikati ya Afrika na Madagascar, kisiwa hiki ni maarufu kama ‘kisiwa cha marashi”