Wakati wakimbizi wa Ronhingya kwenye kambi za Cox’s Bazar na jamii zinazowahifadhinchini Bangladesh wakijiweka tayari kwa msimu wa monsoon unaoambatana na upepo mkali na mvua kubwa, shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM, kwa kushirikiana na serikali ya Bangladesh wapo mstari wa mbele kuhakikisha watu hao wanapata msaada wa hali na mali ili kukabiliana na janga hilo