Joto kali linatarajiwa katika msimu wa kiangazi mwaka huu 2018 kuanzia Juni, Julai na Agosti, huku theluji katika maeneo ya Arctic ikiwa chini ya kiwango cha kawaida.
Katika maadhimisho ya siku ya ndege wahamiaji leo jijini New York Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameihiza dunia kulinda ndege wahamiaji. Kaulimbiu ya maadhimisho hao ni “kwa pamoja tupaze sauti katika utetezi na ulinzi wa ndege wahamiaji”.
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameitaka Poland ihakikishe kila mtu anashiriki ipasavyo mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini humo.