Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameelezea umuhimu wa kupunguza hatari za majanga katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na kufikia malengo ya kuzitoa nchi zinazoendelea katika umasikini.
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, limeonya dhidi ya ongezeko la idadi ya watu wanaohitaji chakula Mashariki mwa eneo la Sahel Afrika Magharibi.
Ripoti ya teknolojia na ubunifu ya UNCTAD ya mwaka huu inaitaka Afrika kufanya mapinduzi ya kuzingatia mazingira ili kufukia lengo muhimu la milenia la kukabiliana na njaa.
Christiana Figuere kutoka nchini Coasta Rica ametajwa kuwa katibu mkuu mtendaji mpya wa kitengo cha Umoja wa Mataifa cha mabadiliko ya hali ya hewa(UNFCCC).