Tabianchi na mazingira

UM: zaidi ya ajali asili 3 800 zilitokea muongo ulopita

Idara ya Umoja wa Mataifa ya kujaribu kupunguza maafa imeeleza kwamba mnamo muongo uliyopita kumekuwepo na ajali asili 3 800 zilizosababisha vifo vya watu 780 000. Idara hiyo inakadiria ajali asili hizo zimesababisha uharibifu wa mali wa kiasi cha dola bilioni 960.

Haiti yakumbwa na tetemeko jingine

Haiti imekumbwa tena na tetemeko kubwa Ijumatano, na kutikisa majengo na kusababisha mtaharuku mkubwa, watu wakikimbia barabarani baada ya kushuhudia mtetemeko mkubwa ulosababisha maafa siku nane zilizopita.

Lazima UM kuendelea na jukumu la mazungumzo ya hali ya hewa

Mkurugenzi mkuu wa Idara ya mazingira ya UM Achim Steiner anasema ni lazima kwa majadiliano ya kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani yabaki chini ya uwongozi wa UM hata ikiwa mkutano wa viongozi wa Copenhagen mwezi Disemba haukufanikiwa kuleta ufumbuzi.

Mataifa ya dunia kusaidia Haiti

Marekani na mataifa mengi ya kigeni yameshaanza kupeleka msaada wa dharura huko Haiti, Rais Barack Obama ameahidi mpango kabambe wa dharura ukatayo ratibiwa vyema kusaidia Haiti.

Maelfu ya watu waathirika na mafuriko makubwa Kenya: OCHA

Mvua kubwa zilizoendelea kunyesha kwa wiki mbili zilizopita zimesababisha mafuriko makubwa, katika maeneo ya Kaskazini, ya kati na magharibi mwa Kenya, na kuathiri watu wapatao elfu 30.

Mkutano wa UNCTAD kutoa wito wa kuchukuliwa hatua dhidi ya kuangamia kwa Bayonuai-(Viumbe Hai)

Zaidi ya watu 500 muhimu kutoka serikali mbalimbali, mashirika ya kimataifa na nyanja ya mitindo na vipodozi watakutana mjini Geneva tarehe 20 na 21 ya mwezi huu wa Januari, ili kutoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kuzuia kuangamia kwa viumbe hai duniani.

Mvua kali zasababisha maelfu ya watu kuathirika Kenya

Afisa wa idara ya umoja wa mataifa juu ya Misaada ya Dharura (OCHA), Bi Elisabeth Byrs amesema kati ya Disemba 27 mwaka 2009 hadi Januari 5 2010 kumekuwepo na mvua kali huko maeneo ya Kaskazini, Kati na Magharibi mwa Kenya , na kuwathiri watu elfu 30.