Tabianchi na mazingira

Mashirika ya UM yaripoti mapigano makali yameshtadi Yemen Kaskazini

Mapigano makali yalioshtadi baina ya vikosi vya Al Houti na majeshi ya serikali Yemen kaskazini, kwenye maeneo ya mji wa Sa\'ada yanaripotiwa kuendelea bila kujali usalama wala hali ya raia wa kawaida.

Mafuriko makali kuipamba Afrika Magharibi na kuathiri 600,000 ziada

Imeripotiwa na Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) ya kwamba mafuriko makali ya karibuni Afrika Magharibi yameathiri watu 600,000 hivi sasa na kusababisha vifo 159.

KM ayasihi Mataifa Wanachama kuharakisha mapatano ya kukomesha uchafuzi wa hali ya hewa

Wiki iliopita KM Ban Ki-moon, alizuru ukingo wa ncha ya Kaskazini ya dunia, kwenye eneo la Akitiki, ambapo alishuhudia mwenyewe athari kubwa za mabadiliko ya hali ya hewa na kujionea, binafsi, namna miamba ya barafu na michirizi ya barafu inavyoyayuka kwa kasi kabisa kwenye eneo hilo, hali ambayo inachochea kina cha bahari kunyanyuka katika sehemu kadha za dunia, na kuhatarisha baadhi ya mataifa ya visiwa ambavyo huenda vikaangamia ikiwa hali hii haotidhibitiwa mapema.

OCHA inasema mafuriko Afrika Magharibi yameathiri watu 350,000

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti Afrika Magharibi inaathiriwa hivi sasa na mafuriko makubwa yaliofumka katika siku za karibuni.

Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro anasailia miaka miwili ya utendaji kazi katika UM

Dktr Asha-Rose Migiro, raia wa Tanzania, alianza kazi rasmi ya NKM wa UM mnamo tarehe mosi Februari 2007. Alikuwa ni NKM wa tatu kuteuliwa kuchukua nafasi hii tangu ilipoanzishwa rasmi katika 1997.

UM waitaka Israel kuruhusu vifaa kuingia Ghaza haraka kufufua huduma za maji

Mratibu wa Misaada ya Kiutu kwenye Maeneo Yailokaliwa Kimabavu ya WaFalastina, Maxwell Gaylard - akijumuika na Jumuiya za Mashirika Yasio ya Kiserikali yanayoambatana na Mashirika ya Kimataifa juu ya Misaada ya Maendeleo - wametangaza leo hii taarifa maalumu yenye kuthibitisha kufanyika uharibifu mkubwa wa vifaa vya huduma za usafi na maji katika eneo la Tarafa ya Ghaza, hali ambayo inazidisha ugumu wa maisha kwa umma wa eneo hili na kuwanyima hadhi yao ya kiutu.

Mkutano wa WCC3 waafikiana kuanzisha mfumo mpya wa kuhudumia utabiri wa hali ya hewa

Mkutano Mkuu wa Tatu juu ya Hali ya Hewa (WCC3) unaokutana hivi sasa Geneva, Alkhamisi ulipitisha Mwito wa Azimio la kuanzisha Mfumo Mpya wa Dunia Kuhudumia Utabiri wa Hali ya Hewa, utaratibu ambao utayawezesha Mataifa Wanachama kupata taarifa, kwa wakati, kuhusu mageuzi katika hali ya hewa.

KM asihi Mkutano wa WCC3 kuharakisha maafikiano ya kudhibiti mageuzi ya hali ya hewa.

Wajumbe kadha wa kimataifa waliokusanyika Geneva, kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tatu juu ya Hali ya Hewa (WCC3) walipata fursa ya kumsikiliza KM Ban Ki-moon akisihi, kwa bidii kuu, juu ya umuhimu wa mataifa kuhakarisha makubaliano ya mkataba mpya wa kudhibiti bora mabadiliko ya hali ya hewa katika dunia.

Uwekezaji wa katika mifumo ya ikolojia una matumaini ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa, inasema TEEB

Matokeo ya mradi ulioanzishwa na Ujerumani pamoja na Kamisheni ya Mataifa ya Ulaya kuhusu masuala ya hali ya hewa, unaosimamiwa na Taasisi juu ya Uchumi wa Mfumo wa Ikolojia na Viumbe Hai Anuwai (TEEB), yamethibitisha dhahiri kwamba uwekezaji kwenye huduma za kufufua mifumo ya ikolojia ni hatua yenye uwezo mkubwa wa kudhibiti bora taathira za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, na ni hatua itakayoimarisha uchumi wa kimataifa, halkadhalika, pindi itatekelezwa kama inavyostahiki.

KM ahimiza mataifa kukamilisha maafikiano ya Mkutano Mkuu juu ya taathira za hali ya hewa

KM Ban Ki-moon amewasihi walimwengu kuchukua hatua za dharura ili kukabiliana haraka na athari chafuzi za mabadiliko ya hali ya hewa, na kuyahifadhi maisha ya vizazi vijavyo.