Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya tabianchi yanahatarisha amani Sahel-ECOSOC

Baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa mataifa ECOSOC kwa ushirikiano na kamisheni ya kujenga amani leo limefanya kikao cha kujadili mabadiliko ya tabianchi na uhusiano wake katika kukwamisha juhudi za ujenzi wa amani  na kudumisha amani katika Ukanda wa Sahel.

Guterres aelezea mshikamano wake na Marekani kufuatia moto jimboni California

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea kusikitishwa kwake kufuatia taarifa za vifo na uharibifu mkubwa kutokana na moto wa nyika unaoendelea kukumba jimbo la California nchini Marekani.

Sekta ya ubunifu wa nguo nayo yahaha kulinda mazingira

Wakati dunia ikihaha kusaka mbinu za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira, sekta ya ubunifu wa mitindo nayo imeshachukua hatua ili kuhakikisha bidhaa zake haziharibu mazingira.

IFAD yawezesha wakulima Chad kuendelea kutumia ufuta kama kiambato kikuu cha mlo

Nchini Chad mradi wa mfumo wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD umesaidia wakulima kukabiliana na matatizo yaliyowakumba katika kilimo cha zao la ufuta linalotegemewa kwa lishe na kipato. Taarifa zaidi na Arnold Kayanda.

Kama ng’ombe wangekuwa nchi, nchi hiyo ingekuwa ya tatu kwa uchafuzi wa mazingira duniani.

Pengine si wengi wanaoiingia katika mghahawa unaouza mathalani burger yaani nyama iliyofunikwa kwa mkate, wanaowaza kuwa chakula hicho wanachokinunua ni sawa na kushiriki katika kuharibu mazingira. Harakati za binadamu katika kutengeneza nyama ni njia mojawapo za uharibifu unaoacha alama duniani.

Tusikose lishe kwa kupoteza na kutupa chakula:FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limetoa wito wa kuhakikisha chakula hakipotei au kutupwa hovyo ili kulinda virutubisho na lishe muhimu kwa ajili ya maisha ya binadamu.

Mizozo inapopamba moto, mazingira nayo huwa hatarini- UNEP

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuzuia uharibifu wa mazingira kwenye maeneo ya mizozo na vita, Umoja wa Mataifa umeweka bayana sababu za kulinda mazingira ikitolea mfano maeneo sita ambako bayonuai imeharibiwa kutokana na vita. 

Vijana waenzi stadi ya ‘Inamura no Hi’ iliyotumika miaka 164 kupunguza janga la tsunami Japan

Mkuu wa ofisi  ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kupunguza athari za majanga, UNISDR, Mami Mizutori amewaeleza wanafunzi wanaokutana katika kongamano la kukuza uelewa kuhusu Tsunami kuwa kupunguza hatari za majanga ni eneo muhimu ambalo linahusu kila taaluma.

Kuimarika kwa tabaka la ozoni ni tija dhidi ya mabadiliko ya tabianchi-UN

Matokeo ya utafiti mpya yalitotolewa leo na ripoti ya Umoja wa Mataifa yanaonyesha kuwa kuendelea kuimarika kwa tabaka la ozoni kumechukuliwa kama mfano wa mafanikioambayo yanayoweza kufikiwa na mikataba ya kimataifa, na kama chagizo la hatua zaidi za kukomesha ongezeko la joto duniani. 

Tsunami ni ‘mwiba’ kwa uhai wa binadamu na uchumi wa nchi- UNISDR

Hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii  kuhusu tsunami, msisitizo ukiwa ni  hasara za kiuchumi, Umoja wa Mataifa unasema idadi ya vifo na hasara za kiuchumi zitokanazo na matukio ya tsunami kwa nchi zinazopakana na bahari ya India na Pasifiki zimeongezeka katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.