Tabianchi na mazingira

Kugawanya manufaa ya genetiki za mimea kusaidia kulinda familia ya mimea iliyo hatarini

Waakilishi wa zaidi ya nchi 60 wakiwemo mawaziri 22 wamekusanyika mjini Rome kwa jitihada mpya za kuunga mkono mkataba wa kimataifa kuhusu genetiki za mimea inayotajwa kuwa muhimu katika kugawanya faida itokanayo na genetiki za mimea kwa chakula na kilimo.

Changamoto za kuwalinda waliohama makwao na wakosa uraia kuongezeka:Guterres

Mkuu wa tume ya wakimbizi ya Umoja wa Mataifa António Guterres ameonya kuwa kunaendelea kushuhudiwa changamoto katika kuwalinda mamilioni ya watu waliolazimishwa kuhama makwao pamoja na wakosa uraia na kuitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dharura.

Ban atoa wito kwa makubaliano mapya ya kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kuafikiwa kwa makubaliano kwenye mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa unaondelea mjini Cancun Mexico na kuwataka wajumbe kwenye mkutano huo kujua kuwa kucheleweshwa kwa makubaliano kunaiweka hatarini afya ya dunia, uchumi wa dunia na pia kwa wanadamu.

Njia ya kuafikia makubaliano ya Cancun yaanza kujitokeza-UM

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa unaondelea mijini Cancun Mexico unaingia wiki yake ya pili ambapo pia ni mkutano wa sita wa nchi wanachama kwenye makubaliano ya Kyoto .

Njia ya kuafikia makubaliano ya Cancun yaanza kujitokeza-UM

Vyombo vya Umoja wa Mataifa vinavyoshughulikia mpango wa uratibuji mazingira vinamatumaini kwamba mkutano wa Cancún, Mexico ambao unajadilia changamoto za mazingira huenda ukifikia makubaliano ya kupitisha azimio jipya hapo Ijumaa.

Mwaka 2010 umevunja rekodi ya joto:WMO

Mwaka huu bila shaka unatarajiwa kushika rekodi ya miongoni mwa miaka mitatu iliyowahi kuwa na joto sana duniani tangu kuanzishwa kwa chomo ya kuweka takwimu za hali ya hewa mwaka 1850, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa duniani WMO.

Upungufu wa fedha kukabili hali ya hewa una athari:FAO

Mafuriko na ukame katika nchi ambazo ni wazalishaji wakubwa wa chakula kwa mwaka huu yamesababisha kupanda kwa bei za chakula, ikiashiria hatari iliyopo katika mfumo wa uzalishaji wa chakula duniani na masoko ya kilimo.

FAO yatoa kitabu kusifia mmea wa mkaukau

Shirikala la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limechapisha kitabu kama ishara ya kusherekea mafanikio ya zao moja ambalo linaweza kustahimili kwenye mazingira ya aiana mbalimbali.

UM wazindua wavuti kusaidia nchi kutekeleza miradi ya mazingira

Umoja wa Mataifa umezindua wa wavuti yaani website ili kuzisaidia nchi zinazoendelea kuwa na njia ya kupata fedha kwa ajili ya kufadhilia miradi inayolenga mazingira.

Teknolojia tofauti ya nishati kupunguza gesi chafu:UNEP

Kwa kuondoa mifumo ya kupata mwangaza isiyostahili mataifa yana uwezo wa kupunguza matumizi yao ya kawi, gesi zinazochafua mazingira na piz kupunguza gharama za kupata mwangaza kwa kutumia taa.