Tabianchi na mazingira

FAO yachukua hatua kupunguza makali ya El Nino kwa wakulima na wafugaji Malawi

Shirika la chakula na kilimo duniani,  FAO kwa usaidizi wa Belgium limeandaa mradi wa kupunguza makali ya madhara ya ukame uliosababishwa na El Nino nchini Malawi mwaka jana wa 2018.

Miaka minne iliyopita ilikuwa na viwango vya juu vya joto kuwahi kushuhudiwa- WMO

Shirika la hali ya hewa duniani, WMO limesema ongezeko la viwango vya joto ni ishara dhahiri ya mabadiliko ya tabianchi ya muda mrefu, huku ikisema miaka minne iliyopita viwango vilikuwa vya kipekee.

EU yatoa dola milioni 6.7 kwa ajili ya shughuli za FAO Yemen.

Wakati amani ya Yemen ikiwa katika hali mbaya na pia kukiwa na uhaba wa chakula, Muungano wa Ulaya na shirika la chakula na kilimo duniani FAO leo mjini Amman, Jordan, wametangaza mchango mpya uliotolewa na muungano wa ulaya wa kiasi cha dola  milioni 6.7 dola katika kuunga mkono kazi ya FAO ya kujenga uwezo wa Yemen kushughulikia masuala yanayosababisha uhaba wa chakula.

Ekari 150 za mashamba ya migomba zateketea kwa moto Torit Sudan Kusini

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini , UNMISS umesema ekari 150 za mashamba ya migomba zimeteketea kwa moto wa nyika kwenye eneo la Iyere Payam katika jimbo la Torit nchini humo.

Viwango vya joto na baridi mwezi Januari vilizidi kipimo- WMO

Shirika la hali ya hewa duniani, WMO limetoa tathmini ya mwenendo wa hali ya hewa katika maeneo mbalimbali ulimwenguni kwa mwezi uliopita wa Januari, tathmini ambayo inaonyesha madhara ya myoto ya nyika, mafuriko na mvua.