Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linasema kuwa maelfu ya ekari ya ardhi ya kilimo pamoja na mazao vimeharibiwa na mafuriko na mvua kubwa katika maeneo ya kunisi mwa Afrika na na kuonya kuwa huenda kukawa na uharibifu mkubwa iwapo viwango hivyo vya mvyua vitaendelea kushuhudiwa.
Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa akiwa mjini Nairobi hii leo amesema changamoto nyingi za kibinadamu zinazoikabili Kenya nyingi zikitokana na kujirudia kwa hali ya ukame na ukuaji wa haraka wa miji zinaweza kushughulikiwa kwa kutumia njia zitakazozihakikishia jamii uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema ukame na sio kutokuwepo kwa usalama sasa ni sababu kubwa inayosambaratisha maelfu ya watu nchini Somalia.
Mchango wa samaki katika mlo wa binadamu duniani umeongezeka sana na kufikia rekodi ya wastani wa kilo 17 kwa mtu mmoja na kuwalisha watu zaidi ya bilioni tatu wakichangia asilimia 15 ya protin ya wanyama inayoliwa na binadamu.
Miezi sita baada ya mafuriko nchini Pakistan mahitaji ya dharura hayaonekani kuisha leo wala kesho huku mamilioni bado wanahitaji msaada kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihutubia kwenye kongamano la kimataifa la uchumi mjini Davos Uswisi amesema ili kuwaondoa watu katika umasikini huku tukilinda mazingira na kuchagiza ukuaji wa uchumi, dunia inahitaji kubadilika.