Tabianchi na mazingira

Madagascar yapigwa na kimbunga cha Bingiza

Kimbunga cha Bingiza kinachosafiri wa umbali wa kilomita 160 kwa saa kimeipiga Madagascar na kuharibu nyumba kadhaa katika jimbo la Mananara.

Norway na Ujerumani zahaidi kutoa fungu la fedha kusaidia FAO kukabili tatizo la mabadiliko ya tabia nchi

Ujerumani na Norway zimehaidi kutoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 5

kusaidia mpango unaoendeshwa na shirika la umoja wa mataifa la chakula na kilimo

FAO ambao inakusudia kusambaza taarifa duniani kote kuhusiana na mradi wa

mapinduzi ya kijani ili kulinda mazingira

Ghana yageukia nyuklia kuwa na uhakika wa nishati

Ghana inageukiwa nyuklia katika kutosheleza mahitaji yake ya nishati yaliyosababishwa na ukuaji wa uchumi na kuendelea kwa viwanda.

UNICEF yawasaidia Wapakistani wanaokabiliwa na baridi:

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linakimbiza misaada muhimu kwa kwa njia ya helkopta kwa maelfu ya Wapakistan walionusurika na mafuriko ambao sasa wako katika hatari kutokana na msimu wa baridi kali.

WFP inaongeza msaada Sri Lanka baada ya athiri za mafuriko

Kwa mara ya pili katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja mvua kubwa za monsoon zimewalazimisha maelfu ya watu kuzikimbia nyumba zao nchini Sri Lanka baada ya kusababisha mafuriko katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

Hatua zikichukuliwa kupunguza majanga maisha yatanusurika:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza kwenye mkutano huo wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa amesema mwaka jana ulighubikwa na majanga.

Nchi zinazoendelea zimetakiwa kuwekeza katika kuzuia na kupunguza majanga:UM

Nchi zinazoendelea zimetakiwa kuwa na ari ya kisiasa ya kuwekeza katika mipango ya kupunguza au kuzuia majanga.

Mafuriko yaliyozuka tena Sri Lanka yamesababisha athari kubwa:OCHA

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema mafuriko ya awamu ya pili nchini Sri Lanka yamesababisha athari kubwa kuliko ya kwanza.

Mafuriko Sri Lanka yameleta athari kubwa:OCHA

Nchini Sri Lanka, mvua kubwa zilizonyesha katika siku saba zilizopita zimesababisha mafuriko katika wilaya 18 zikiwemo za Mashariki, Kaskazini, Katikati, Uva na majimbo ya Kusini .

Serikali ya Sudana na UNAMID kufanya mkutano wa kimataifa wa maji Darfur

Jimbo la Darfur Sudan linakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji suala ambalo linaonekana kuwa moja ya sababu ya machafuko ya kikabila hasa kutoka jamii za wakulima na wafugaji.