Tabianchi na mazingira

UNICEF itaandaa warsha maalumu Copenhagen, kwa watoto kuzingatia mageuzi ya hali ya hewa

Warsha Maalumu wa Watoto Kuzingatia Masuala juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani unaandaliwa kufanyika kwenye mji wa Copenhagen kuanzia Novemba 28 mpaka Disemba 04 (2009), kabla ya Mkutano Mkuu wa UM juu ya Udhibiti wa Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa kuanza majadiliano.

Viwango vya gesi chafuzi duniani vinaripotiwa kufurutu ada

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) kwenye ripoti yake mpya iliochapisha Ijumatatu, imeeleza kwamba kiwango cha ile hewa chafu inayotupwa kwenye anga, kinaeendelea kukithiri katika dunia.

Mazungumzo ya Redio ya UM na mshindi wa mashindano ya picha ya UNDP/Olympus/AFP kutoka Kenya

Ijumatano raia wawili wa kutoka Kenya, pamoja na mzalendo mwanamke kutoka Morocco, walitunukiwa zawadi maalumu, kwa picha zao zilizoonyesha namna watu wa kawaida barani Afrika, wanavyoshiriki kwenye harakati za kutunza na kuhifadhi mazingira - ikijumlisha zile shughuli za kupandisha miti, na huduma za kuigeuza mifuko ya plastiki, iliotupwa kwenye majaa baada ya kutumiwa, kuwa mikoba ya pochi na vikapu, ikiwa miongoni mwa kadhia muhimu zinazochangia kimataifa katika kupunguza athari haribifu za mabadiliko ya hali ya hewa.

Natija za ubora wa hewa zitasailiwa kwenye Mkutano wa Sayansi ya Angahewa utakaofanyika Korea Kusini

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limearifu ya kuwa kikao cha kumi na tano cha Kamisheni juu ya Sayansi ya Angahewa, kitaanzisha mijadala maalumu mnamo siku ya Ijumatano, katika Korea Kusini.

Viongozi wa kimataifa wameakhirisha jukumu la kukamilisha itifaki ya Copenhagen juu ya mabadiliko ya hali ya hewa

Imeripotiwa hii leo kwamba viongozi wa kimataifa wameafikiana kuakhirisha yale majadiliano ya kufikia mapatano juu ya mabadiliko ya hali ya hewa katika mkutano ujao utakaofanyika mwezi Disemba katika Copenhagen, na badala yake wamekubaliana kwamba mkutano huu wa mabadiliko ya hali ya hewa ujaribu kufikia itifaki isio na uzito "wenye masharti ya kisiasa" ili kuwawezesha wajumbe wa kimataifa kuhakikisha masuala magumu yenye kutatanisha majadiliano yao yatazingatiwa kidhati katika siku za baadaye.

UNFPA itawasilisha ripoti mpya wiki ijayo juu ya idadi ya watu duniani

Ijumatano ijayo, tarehe 18 Novemba, Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) itawasilisha ripoti mpya kuhusu uhusiano wa mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake kwa wanawake.

Treni ya 'Climate Express' inaelekea Copenhagen kumurika umuhimu wa kuhitimisha mapatano ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

Wanaharakati 400 ziada juu ya mabadiliko ya hali ya hewa, wakijumlisha wapatanishi, viongozi wa mashirika ya kibiashara pamoja na watetezi wa hifadhi ya mazingira wanatarajiwa kusafiri pamoja kwenda Copenhagen kwa treni yenye jina la ‘Treni ya Hali ya Hewa ya Haraka\' (Climate Express), kwa madhumuni ya kuwahimiza viongozi wa dunia kufikia makubaliano yalio ya haki, yenye masharti ya kisheria na nia ya kutekelezwa, pale watakapokusanyika Denmark kuhudhuria mkutano mkuu wa UM juu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Viongozi wa dunia wahimizwa na KM kuhudhuria Mkutano wa Copenhagen ili kuwasilisha mapatano ya kuridhisha

Mapema Alkhamisi Msemaji wa KM alitoa taarifa maalumu kwa waandishi habari, kuhusu Mkutano Mkuu ujao wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa, utakaofanyika mjini Copenhagen.

Suluhu hakika yahitajika kudhibiti upungufu wa maji unaosababishwa na hali ya hewa ya kigeugeu

Wiki hii tunajadilia umuhimu wa kuzingatia, kwa kina, mchango wa maji safi na salama, katika udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa.

OCHA yaripoti watu 16,000 wang'olewa makazi Usomali na mafuriko

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti, kwa akali, watu 16,000 waling\'olewa makazi kwa sababu ya mafuriko katika majimbo ya Usomali ya Hiraan, Gedo na Shabelle ya Chini.