Tabianchi na mazingira

Ripoti fupi kuhusu matukio ya Mkutano Mkuu wa Copenhagen

KM Ban Ki-moon amenakiliwa akifuatilia, kwa ukaribu zaidi, hekaheka na harakati za kijumla kwenye Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya hewa, wakati majadiliano yakipamba na kuendelea miongoni mwa wajumbe wa kimataifa.

Wawakilishi wa G-77 waamini kuna rasilmali za kutosha ulimwenguni kukomesha madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa

Wawakilishi wa Mataifa wanachama wa Kundi la G-77 na Uchina, wamesisitiza kwenye kauli kadha walizowasilisha kwenye majadiliano ya Copenhagen ya kuwa umma wa kimataifa, kwa ujumla, katika karne ya ishirini na moja, umebarikiwa rasilmali ya kutosha kushughughulikia, kwa mafanikio, matatizo

KM awaambia wajumbe wa Mkutano juu ya Mfuko wa CERF "twahitajia misaada zaidi kukabili athari za gesi chafuzi"

Asubuhi kwenye Makao Makuu, kulifanyika kikao maalumu kuzingatia shughuli za ile Taasisi ya Mfuko wa UM juu ya Maafa ya Dharura au Mfuko wa CERF.

Wataalamu wa kimatafia wanajiandaa kubuni viashirio vipya juu ya mifumko ya ukame duniani

Kuhusu athari za mabadiliko ya hali ya hewa zilizoshuhudiwa kutukia ulimwenguni mnamo miaka ya karibuni, Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani, (WMO), limebashiria kutatukia muongezeko mkubwa wa marudio ya ukame mkali, katika sehemu mbalimbali za dunia katika miaka ijayo.

Waraka wa siri uliofichuliwa Copenhagen waonyesha mgawanyo wa matarajio kati ya nchi tajiri na zile zenye maendeleo haba

Majadiliano ya Mkutano wa UM juu ya taratibu za kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, Ijumanne yalikabiliwa na mtafaruku na vurugu lisiotarajiwa, baada mataifa yanayoendelea kuonyesha ghadhabu kubwa juu ya waraka wa siri uliofichuliwa na vyombo vya habari,

Halijoto duniani, kwa mwongo wa 2000, imefurutu kawaida, imehadharisha WMO

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limetangaza ripoti iliobainisha, kihakika, kwamba mwaka 2009 ni miongoni mwa vipindi 10 vilivyoshuhudia kiwango kikubwa kabisa cha halijoto katika dunia, kuanzia 1850, mwaka ambao WMO ulipoanzisha ukusanyaji wa takwimu juu ya kumbukumbu ya halijoto.

Uchina inahimiza nchi tajiri kutimiza haraka ahadi za kupunguza utoaji wa gesi joto na haribifu kwenye anga

Kwa upande mwengine, mjumbe wa Uchina, alitoa mwito maalumu kwa zile nchi zenye maendeleo ya viwanda, unaozihimiza kutimiza, kwa uaminifu, ahadi walizotoa siku za nyuma na kuongoza kwenye kadhi ya kupunguza utoaji wa hewa chafu kwenye anga, kwa viwango vilivyo vikubwa,

Mkuu wa UM kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa, ahimiza wapatanishi kuandaa kidharura marekibisho ya kifedha na kitaaluma kumudu bora athari za gesi chafuzi

Yvo de Boer, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya UM ya Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC) kwenye mahojiano aliofanya Ijumanne na waandishi habari, alisema ufunguzi wa Mkutano Mkuu ulianza kwa "hatua ya kutia moyo, na katika nafasi muafaka,

KM ana matumaini juu ya itifaki ya kupunguza utoaji wa gesi chafu angani

KM Ban Ki-moon kwenye mahojiano na gazeti la kila siku la Denmark, linaloitwa Berlingske Tidende - yaliochapishwa Ijumapili, alisema ana "matarajio ya matokeo mazuri kutokana na majadiliano ya wawakilishi wa kimataifa" kwenye mkusanyiko wa Copenhagen.

Mashirika ya UM yamehadharisha kuhusu tofani Bukini

Mashirika ya UM yametangaza kuwa na wasiwasi juu ya kunyemelea kwa majira ya matofani na vimbunga katika taifa la Bukini, maafa ambayo kama hayajadhibitiwa yanaashiriwa huenda yakaathiri maisha ya watu 600,000.