Tabianchi na mazingira

UNEP inahimiza uwekezaji wa mazingira uongezwe kuimarisha uchumi wa dunia

Ripoti iliotolewa Ijumatatu na Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) imebainisha awamu ya tatu ya furushi la mradi wa kuwekeza dola trilioni 2 na nusu, zinazohitajika kufufua uchumi wa dunia unaofungamana na mazingira bora, yalio safi na salama.

KM ahimiza mataifa kujumuika kudhibiti kidharura mabadiliko ya hali ya hewa

KM Ban Ki-moon anahudhuria Mkutano Mkuu juu ya Maendeleo ya Kusarifika, unaofanyika mjini New Delhi, Bara Hindi ambapo aliwaambia wajumbe wa kimataifa waliokusanyika huko ya kuwa walimwengu wanawajibika kukabili, kipamoja, tishio hatari, linaloendelea kupanuka kimataifa, linalochochewa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Wajumbe wa kimataifa wakutana Roma kuandaa miradi ya kudhibiti bora maji duniani

Wajumbe wa kimataifa kutoka nchi 60 ziada wanakutana mjini Roma, Utaliana kwenye Makao Makuu ya Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) kuanzia leo tarehe 21 mpaka 23 Januari (2009) ambapo wataendelea kujadiliana mpango wa utendaji, unaohitajika kudhibiti bora matumizi ya maji ulimwenguni, kufuatia athari mbaya za mazingira zinazochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.