Mabadiliko ya Tabianchi

Mawasiliano ya simu za mikononi yatazamiwa kuhamasisha mapinduzi kwwenye utabiri wa hali ya hewa Afrika

Baraza juu ya Misaada ya Kiutu Duniani, na Raisi wake, KM wa UM mstaafu Kofi Annan, akijumuika na kampuni ya mawasiliano ya Ericsson, Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO), na vile vile kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi, Zain, pamoja na Taasisi ya Huduma za Maendeleo Duniani ya Chuo Kikuu cha Columbia, Marekani wote pamoja wametangaza, leo hii, taarifa ya kufadhilia mradi mkuu, unaojulikana kama "Mradi wa Taarifa za Hali ya Hewa kwa Wote", ambao ukitekelezwa una matumaini ya kuwasilisha mapinduzi ya kuridhisha katika kuimarisha zaidi uwezo wa kusimamia mtandao wa utabiri wa hali ya hewa, hususan kwenye yale mazingira yanayoendelea kuathiri hali ya hewa barani Afrika.

Siku ya Dunia Kupiga Vita Kuenea kwa Jangwa

Tangu 1995 UM unaihishimu tarehe 17 Juni, kila mwaka, kuwa ni Siku ya Kupiga Vita Kuenea Kwa Jangwa. Ripoti za UM juu ya tatizo la kueneza majangwa, kutokana na matumizi badhirifu ya ardhi, inaashiria watu milioni 200 watalazimika kuhama makazi katika mwaka 2050 kutakakosababishwa na mabadiliko ya katika mazingira.

Maendeleo kupatikana kwenye mkutano wa kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

Mkutano wa UM uliofanyika Bonn, Ujerumani mwezi huu, kuzingatia masuala yanayohusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani, umemalizika Ijumaa ya leo na iliripotiwa kumepatikana mafanikio ya kuridhisha katika maandalizi ya waraka wa ajenda ya majadiliano, kwa kubainisha dhahiri matarajio ya serikali wanachama kutoka Mkutano ujao wa Copenhagen, ili kuharakisha udhibiti bora wa taathira za mabadiliko ya hali ya hewa kimataifa.

Nabarro ahadhirisha, afya isiotunzwa ya mifugo huathiri wanadamu kwa mapana na marefu

Mratibu wa Mradi wa UM Kupambana na Homa za Mafua na Mzozo wa Chakula Duniani, Dktr David Nabarro, amenakiliwa akihadharisha, kutokea Vienna, Austria ya kwamba afya ya mifugo ni muhimu sana katika kudumisha maisha bora kwa wanadamu.

Mashirika ya huduma za kiutu yataka kuanzishwe miradi ya kuhifadhi raia na athari za mabadiliko ya hewa

Mashirika 18 ya UM yenye kuhudumia misaada ya kiutu, yakichanganyika na mashirika wenzi mengineyo yalio wanachama wa ile Kamati ya Kudumu ya Jumuiya Zinazotegemeana (IASC), yamependekeza kujumuishwa kwenye mkataba utakaofuatia Mkataba wa Kyoto, yale masuala yanayohusu athari haribifu dhidi ya wanadamu, zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

UNEP kuanzisha mradi mpya kuhishimu wajasiri wa kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limeanzisha mradi maalumu wa kuihishimu ‘Siku ya Mazingira Duniani’ utakaowatambua wale watu wanaoshiriki kwenye juhudi mbalimbali za uvumbuzi mpya na usio wa kawaida wa kuamsha hisia za umma kutunza mazingira.

Siku ya Mazingira Duniani

Siku ya leo, tarehe 05 Juni (2009) huadhimishwa kila mwaka na UM kuwa ni \'Siku ya Mazingira Duniani\'. Lengo hasa la siku hii ni kuendeleza mwamko unaofaa, miongoni mwa umma wa kimataifa, kuhusu mazingira, kwa ujumla, na kufahamishana hatari inayokabili maumbile haya, na pia kuwahamasisha wanadamu kuwa mawakala wa kuwasilisha mabadiliko yatakayosaidia kuhifadhi mazingira na kudumisha maendeleo.

IFAD inayahimiza mataifa Afrika kukipa kilimo umuhimu kupambana na matatizo ya fedha

Kanayo F. Nwanze, Raisi wa Shirika la UM linalohusika na ukomeshaji wa ufukara na umaskini wa vijijini, yaani Shirika la Kimataifa juu ya Maendeleo na Kilimo (IFAD) ameshauri kwamba serikali za Afrika, zenye kutunza na kuhudumia kimaendeleo sekta ya kilimo, ndizo zitofanikiwa kudhibiti, kwa wastani, athari mbaya zinazoletwa na migogoro ya fedha duniani.

BK kupitisha azimio la kutiaka UM kuchunguza athari hatari ya mabadiliko ya hali ya hewa dhidi ya usalama

Ijumatanao, Baraza Kuu (BK) la UM, kwenye kikao cha wawakilishi wote lilipitisha, kwa kauli moja, azimio lenye kuyahimiza mashirika na taasisi zote za UM kufanya uchunguzi wa kuzingatia uwezekano wa kuzuka madhara haribifu dhidi ya usalama na amani duniani, kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, pindi jumuiya ya kimataifa itashindwa kuyadhibiti maafa hayo mapema.

Huduma za kilimo ni muhimu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani: FAO

Juhudi za kufarajia maendeleo yanayosarifika kwenye sekta ya kilimo, hasa katika nchi zinazoendelea, ndio kadhia muhimu pekee yenye uwezo wa kudhibiti bora mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa duniani, na katika kupunguza njaa na ufukara, imeeleza Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO).