Mabadiliko ya Tabianchi

Siku ya Mazingira Duniani

Siku ya leo, tarehe 05 Juni (2009) huadhimishwa kila mwaka na UM kuwa ni \'Siku ya Mazingira Duniani\'. Lengo hasa la siku hii ni kuendeleza mwamko unaofaa, miongoni mwa umma wa kimataifa, kuhusu mazingira, kwa ujumla, na kufahamishana hatari inayokabili maumbile haya, na pia kuwahamasisha wanadamu kuwa mawakala wa kuwasilisha mabadiliko yatakayosaidia kuhifadhi mazingira na kudumisha maendeleo.

IFAD inayahimiza mataifa Afrika kukipa kilimo umuhimu kupambana na matatizo ya fedha

Kanayo F. Nwanze, Raisi wa Shirika la UM linalohusika na ukomeshaji wa ufukara na umaskini wa vijijini, yaani Shirika la Kimataifa juu ya Maendeleo na Kilimo (IFAD) ameshauri kwamba serikali za Afrika, zenye kutunza na kuhudumia kimaendeleo sekta ya kilimo, ndizo zitofanikiwa kudhibiti, kwa wastani, athari mbaya zinazoletwa na migogoro ya fedha duniani.

BK kupitisha azimio la kutiaka UM kuchunguza athari hatari ya mabadiliko ya hali ya hewa dhidi ya usalama

Ijumatanao, Baraza Kuu (BK) la UM, kwenye kikao cha wawakilishi wote lilipitisha, kwa kauli moja, azimio lenye kuyahimiza mashirika na taasisi zote za UM kufanya uchunguzi wa kuzingatia uwezekano wa kuzuka madhara haribifu dhidi ya usalama na amani duniani, kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, pindi jumuiya ya kimataifa itashindwa kuyadhibiti maafa hayo mapema.

Huduma za kilimo ni muhimu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani: FAO

Juhudi za kufarajia maendeleo yanayosarifika kwenye sekta ya kilimo, hasa katika nchi zinazoendelea, ndio kadhia muhimu pekee yenye uwezo wa kudhibiti bora mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa duniani, na katika kupunguza njaa na ufukara, imeeleza Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO).

Mazungumzo ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa yaanza rasmi Bonn

Duru ya pili ya Mazungumzo ya UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani imeanza rasmi majadiliano Ijumatatu ya leo, kwenye mji wa Bonn, Ujerumani ambapo kutazingatiwa, kwa mara ya kwanza, waraka wa ajenda iliofikiwa na nchi wanachama karibuni, ya kudhibiti bora taathira za mageuzi ya mazingira yanayoletwa na hali ya hewa ya kigeugeu.