Mabadiliko ya Tabianchi

Akiwa COP24 Guterres ataja mambo manne muhimu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 24 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP24 huko Katowice, Poland hii leo na kutaja mambo makuu manne anayoamini ni muhimu ili kubadili mwelekeo wa sasa wa tabianchi.

Hatua ya China na Ufaransa kuelekea COP24 ni ya kipekee- Guterres

Umoja wa Mataifa umepongeza hatua ya Ufaransa na China ya kuchukua dhima ongozi kuelekea mkutano wa 24 wa mabadiliko ya tabiachi huko Poland, hatua ambayo umoja huo imesema inatia matumaini kwa mamilioni ya watu wanaokumbwa na madhara tabianchi hivi sasa.

Matumizi endelevu ya bahari yaangaziwa Nairobi

Mkutano wa kimataifa kuhusu matumizi endelevu ya bahari kwa ajili ya ukuaji wa uchumi ukiingia siku ya pili hii leo huko Nairobi, Kenya, mwakilishi wa serikali ya Zanzibar kutoka Tanzania amezungumzia umuhimu wa bahari katika uchumi wa visiwa hivyo. 

Taarifa sahihi za tabianchi zaokoa wakulima na wafugaji nchini Zambia

Nchini Zambia mradi wa kuwawezesha wakulima na wafugaji kupata taarifa sahihi kuhusu hali ya hewa, umewajengea upya imani baada ya mabadiliko ya tabianchi kuleta misukosuko katika shughuli zao za kilimo na ufugaji. 

Kutoka chupa za plastiki hadi ala za muziki Kibera:UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP linasema kila mbinu ni lazima itumike ili kupambana na plastiki ambazo athari zake ni kubwa sio tu kwa mazingira bali kwa mukstakabali wa binadamu na viumbe wengine baharini na nchi kavu. Na kwa mantiki hiyo limekuwa likichagiza juhudi mbalimbalimbali na ubunifu wa kugeuza taka hizo za plastiki kuwa faida katika jamii  jambo ambalo limeanza kupokelewa kwa mikono miwlili katika sehemu mbalimbali duniani.

Mradi wa matokeo ya haraka Mali waleta kicheko kwa wafugaji Gao

Nchini Mali, mradi wa kiwanda cha maziwa uliofadhiliwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo MINUSMA umesaidia wafugaji na wazalishaji wa maziwa kuinua siyo tu vipato vyao bali pia kuimarisha uhusiano na utangamano baina yao. Taarifa zaidi na Arnold Kayanda.

IFAD yawezesha wakulima Chad kuendelea kutumia ufuta kama kiambato kikuu cha mlo

Nchini Chad mradi wa mfumo wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD umesaidia wakulima kukabiliana na matatizo yaliyowakumba katika kilimo cha zao la ufuta linalotegemewa kwa lishe na kipato. Taarifa zaidi na Arnold Kayanda.

Mizozo inapopamba moto, mazingira nayo huwa hatarini- UNEP

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuzuia uharibifu wa mazingira kwenye maeneo ya mizozo na vita, Umoja wa Mataifa umeweka bayana sababu za kulinda mazingira ikitolea mfano maeneo sita ambako bayonuai imeharibiwa kutokana na vita. 

Kuimarika kwa tabaka la ozoni ni tija dhidi ya mabadiliko ya tabianchi-UN

Matokeo ya utafiti mpya yalitotolewa leo na ripoti ya Umoja wa Mataifa yanaonyesha kuwa kuendelea kuimarika kwa tabaka la ozoni kumechukuliwa kama mfano wa mafanikioambayo yanayoweza kufikiwa na mikataba ya kimataifa, na kama chagizo la hatua zaidi za kukomesha ongezeko la joto duniani. 

Tsunami ni ‘mwiba’ kwa uhai wa binadamu na uchumi wa nchi- UNISDR

Hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii  kuhusu tsunami, msisitizo ukiwa ni  hasara za kiuchumi, Umoja wa Mataifa unasema idadi ya vifo na hasara za kiuchumi zitokanazo na matukio ya tsunami kwa nchi zinazopakana na bahari ya India na Pasifiki zimeongezeka katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.