Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP inatoa muongozo wa jinsi ya kushughulikia changamoto kubwa tatu za dharura zinazoikumba dunia ambazo ni mabadiliko ya tabianchi, kuishi vyema na mazingira na ufikiaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs.
Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, nchini Msumbiji Maria Luisa Fornara akitembelea eneo la Guara Guara ambayo sasa ni makazi ya walioathiriwa na kimbunga Eloise, amesema inasikitisha kuona watoto wakiteseka kwa mara nyingine kutokana na matokeo mabaya ya mabadiliko ya tabianchi.
Kutana na mkulima kutoka Zimbabwe ambaye kupitia miradi ya shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO anajaribu kwa kila njia kuhakikisha mfumo wa kilimo unaboreka lakini pia wakulima wa jamii yake wanalinda mazingira na kuishi kwa amani na wanyamapori.
Nchini Msumbiji, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia manusura wa kimbunga Eloise kilichopiga eneo la Beira jimboni Sofala mwishoni mwa mwezi uliopita ambapo sasa manusura waliokumbwa na mafuriko wanajengewa makazi ya muda sambamba na kuwekewa huduma za kujisafi na maji safi.
Mwaka 2020 ulikuwa ni mwaka wa majanga lakini 2021 ni mwaka wa fursa na matumaini! Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyotoa leo kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani akielezea vipaumbele vyake 10 kwa mwaka 2021.
Nchini Vietnam, mfuko wa maendeleo ya Umoja wa Mataifa, IFAD umesaidia wakulima kuondokana na tabia ya kuonja maji ya umwagiliaji ili kutambua kiwango cha chumvi na badala yake sasa wanatumia teknolojia ya simu ya kiganjani ili kuongeza mavuno ya mpunga
Nchini Brazil, baada ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 kusababisha vifo vya watu zaidi ya 200,000 na hali ya kutoweka kwa misitu ikishika kasi, familia, ndugu na jamaa zimeibuka na mpango wa kupanda miti 200,000 kama njia ya kukumbuka wapendwa wao.
Mwaka 2020 ulikuwa ni miongoni mwa miaka mitatu yenye joto zaidi kuwahi kurekodiwa huku ukichukua nafasi ya tatu baada ya mwaka 2016 kwa mujibu wa takwimu kupitia vipimo tano tofauti za shirika la Umoja wa utabiri wa hali ya hewa WMO.
Karibu robo tatu ya mataifa kote duniani yameweka mipango ya kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi, lakini ufadhili na utekelezaji unaohitajika wa mipango hiyo ndio mtihani mkubwa kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP.
Miaka mitatu mfululizo ya ukame pamoja na kuporomoka kwa uchumi kutokana na ugonjwa wa virusi vya corona au COVID-19 huenda kukaacha theluthi moja ya wakazi wa kusini mwa Madagascar bila uwezo wa kupata mlo limesema Shirika la Umoja wa Matiafa la mpango wa chakula duniani, WFP.