Tabianchi na mazingira

Mkutano wa mwaka wa IAEA umefunguliwa rasmi Vienna

Mkutano Mkuu wa Mataifa Wanachama 145 wa Shirika la Kimataifa juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Kinyuklia (IAEA), utakaochukua wiki nzima, umefunguliwa rasmi mjini Vienna Ijumatatu ya leo.

Wasafishaji mabomu yaliotegwa Lebanon Kusini watunukiwa Tunzo ya NANSEN na UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetangaza leo kwamba litatunukia zawadi yake kuu, inayojulikana kama Tunzo ya Nansen, Tawi la Taasisi ya UM Inayoongoza Shughuli za Kusafisha Mabomu Yaliotegwa Ardhini katika Lebanon Kusini.

KM awasili kazini kwa gari ya nishati ya sola

KM leo asubuhi aliwasili kazini kwa gari maalumu yenye kutumia nishati ya sola, ambayo iliendeshwa kutokea nyumbani kwake mjini New York hadi jengo la Makao Makuu ya UM. Kadhia hii ni moja katika juhudi za KM za kuamsha hisia za umma wa kimataifa juu ya majukumu tuliyonayo kuhibiti bora mabadiliko ya hali ya hewa, na umuhimu wa kuhifadhi mazingira kwa kutumia teknolojia inayotunza mazingira hayo badala ya kuyadhuru.

IAEA inaashiria kuongezeka kwa matumizi ya umeme unaozalishwa na nyuklia katika miaka ijayo

Ripoti iliochapishwa rasmi na Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA), na kutangazwa Alkhamisi (11/09/08) ilibashiria ya kwamba matumizi ya nishati ya nyuklia duniani yataongezeka kwa mara mbili zaidi katika miongo miwili ijayo, kushinda kima cha hivi sasa, kwa sababu ya kukithiri kwa mahitaji ya nishati ulimwenguni.

Ubashiri wa hali ya hewa ni muhimu kupunguza umasikini na kutunza rasilimali ya maji

Michel Jarraud, Mkurugenzi wa Shirika la UM juu ya Upimaji wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) aliwaambia wawakilishi waliohudhuria Mkutano wa Dunia juu ya Maji unaofanyika kwenye mji wa Montpellier, Ufaransa kwamba ni muhimu kwa nchi wanachama kutumia ujuzi wa kisasa wa kutabiri hali ya hewa wakati wanapoandaa miradi ya maendeleo ya uchumi na kupunguza umaskini unaochochewa na athari kubwa za mabadiliko ya hali ya hewa, hususan wanapotathminia akiba ya maji.

UNEP imenasihi ajali zisokwisha za kimaumbile zaweza kukomeshwa panapo udhibiti bora wa hali ya hewa

Achim Steiner, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) leo ametoa taarifa iliohadharisha kwamba pindi mabadiliko ya hali ya hewa yatashindwa kudhibitiwa kama inavyostahiki kisayansi, kuna hatari ya maaafa ya kimaumbile kukithiri na kuathiri kihali na mali umma wa kimataifa, kama ilivyotukia wiki hii katika mji wa New Orleans, Marekani ambapo Kimbunga Gustav kilisababisha maelfu ya watu kuhamishwa makwao na kupelekwa kwenye maeneo salama.

Mataifa ya Afrika kusaidiwa kudhibiti bora hewa safi

Benki Kuu ya Dunia imetoa ripoti maalumu yenye kumurika suala la uwezo wa Afrika kudhibiti vizuri zaidi Mradi wa Maendeleo Safi (CDM) kwa kupunguza ile hewa chafu inayomwagwa kwenye anga kutokana na harakati za viwandani na pia kutoka kwenye magari.