Tabianchi na mazingira

Ripoti ya OCHA/CARE imewakilisha orodha ya mataifa yanayohatarishwa na vurugu la kimazingira

Ripoti iliodhaminiwa na Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) pamoja na shirika lisio la kiserikali linalohudumia misaada ya kiutu la CARE imewasilisha orodha mpya ya maeneo ya kimataifa ambayo yanabashiriwa yatakabiliwa na hatari ya vurugu la kimazingira katika miongo ijayo, mathalan, ukame mbaya, mafuriko yasio kikomo na pia vimbunga vikali.

Fungamano za madhara ya mazingira na afya kuzingatiwa na mawaziri wa Afrika Gabon

Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP), kwa ushirikiano na Serikali ya Gabon wametayarisha, kwa mara ya kwanza Mkutano wa Mawaziri juu ya Fungamano za Afya na Mazingira katika Afrika utakaofanyika wiki ijayo kwenye mji mkuu wa Libreville, Gabon kuanzia tarehe 26 hadi 29 Agosti (2008).

Majadiliano ya kina yameanza Ghana kusailia mkataba wa kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa duniani

Wawakilishi 1,600 kutoka nchi wanachama 160 wamekusanyika hivi sasa kwenye mji wa Accra, Ghana kuhudhuria kikao cha wiki moja (21-27 Agosti 2008)kujadilia nidhamu za kuchukuliwa kipamoja kudhibiti bora tatizo la hewa chafu inayomwagwa angani, tatizo ambalo limethibitika kuwa ndio lenye kuharibu mazingira na kutifua mabadiliko ya kigeugeu ya hali ya hewa kimataifa. Mkutano umeandaliwa na Taasisi ya UM juu ya Mfumo wa Mkataba wa Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani (UNFCCC).

UN-HABITAT imetia sahihi makubaliano ya UM kushiriki kwenye Maonyesho ya Dunia ya Shanghai 2010

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Makazi (UN-HABITAT) yaani Anna Tibaijuka mapema wiki hii ametia sahihi maafikiano maalumu nchini Uchina yatakayoiwezesha UM na mashirika yake kadha kushiriki kwenye Maonyesho Makuu ya Dunia ya Shanghai katika 2010, maonyesho ambayo yatalenga zaidi nidhamu mpya za kuimarisha miji na maendeleo.

Yao Ming ameteuliwa Mshindi wa Kwanza wa UNEP

Mwanariadha wa Olimpiki na ambaye pia mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu kutoka Uchina, Yao Ming ametangazwa kuwa ni Mshindi wa Kwanza wa Tunzo ya Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP). Tangazo hili lilitolewa Ijumamosi kwenye mji wa Beijing.

Naibu mkurugenzi wa IAEA anazuru Iran

Naibu Mkurugenzi wa Shirika la IAEA, Olli HEINONEN, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Usalama amewasili Teheran Alkhamisi, kwa ziara maalumu ya siku mbili. Anatarajiwa kuongoza mazungumzo na maofisa wa vyeo vya juu wa Iran wanaohusika na sera za matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia.~

WMO kusaidia utabiri wa hali ya hewa katika Olimpiki ya Beijing 2008

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limetangaza kuisadia Uchina kutabiri vizuri zaidi hali ya hewa wakati mashindano ya olimpiki yanapopamba katika mji wa Beijing kuanzia tarehe 08 Agosti (08).

Sampuli za 'plutonium' kudhibitiwa baada ya kuvuja kwenye lebu ya IAEA

Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Kinyukilia Kimataifa (IAEA) limeripoti Ijumapili kijichupa kidogo kilichofungwa kwenye maabara ya kuhifadhia sampuli za utafiti na ukaguzi, iliopo kwenye mji wa Seibersdorf, Austria kilifura shinikizo na kuvuja ile sumu kali ya maadini yanayojulikana kama plutonium, ambayo hutumiwa kutengenezea silaha za nyuklia.

UNEP imeshirikiana na Uchina kuandaa Olimpiki rafiki kwa mazingira

Achim Steiner, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) anatarajiwa kuhudhuria Sherehe za Ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki mjini Beijing, Uchina mnamo tarehe 08 Agosti (08). Ziara hii ni kuthibitisha uungaji mkono wa UNEP zile juhudi za Uchina kuendesha mashindano ya olimpiki kwa kulingana na taratibu za kuimarisha hifadhi bora ya mazingira.

IAEA imeidhinisha usalama wa viwanda vya nyuklia India

Bodi la Magavana wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) lilikutana mjini Vienna Ijumaa kuzingatia Mapatano juu ya Ukaguzi Kuhusu Usalama wa Viwanda vya Nishati ya Nyuklia kwa Raia katika India.