Tabianchi na mazingira

'UM uliopoa' kutunza mazingira Makao Makuu

Kuanzia Ijumaa tarehe mosi Agosti, UM utatekeleza mradi maalumu kwenye majengo ya Makao Makuu yaliopo New York, kwa matarajio ya kuongeza akiba ya fedha za matumizi na kutunza mazingira. Hatua hii inachukuliwa kwa kulingana na juhudi za kimataifa za kukabiliana na matatizo yanayotokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, na UM imeamua kuongoza kwenye juhudi hizi kwa vitendo.

Wakulima wanahimizwa kujiunga na mapinduzi ya "Kijanikibichi"/Kilimo

Wajumbe karibu 100 kutoka nchi 36 wanaokutana kwenye Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo (FAO)Roma, Utaliana wiki hii wametoa mwito maalumu wenye kupendekeza kwa wakulima wa kimataifa kujihusisha na yale mapinduzi ya kilimo yanayoendelea, yajulikanayo kama mapinduzi ya "Kijanikibichi". Mapinduzi haya huwakilishwa na utaratibu unaojulikana kama "Mfumo wa Hifadhi Bora ya Ukulima" au Mfumo wa CA.

UM kutetea waathiriwa wa zilzala Uchina kupata misaada ziada ya kihali

Khalid Malik, Ofisa Mkaazi anayehusika na huduma za dharura Uchina, ametangaza kutokea mjini Beijing ya kwamba UM umeanzisha kampeni maalumu ya kuchangisha msaada wa dola milioni 33.5 wa kuwahudumia waathiriwa wa zilzala ya nguvu iliyotukia Mei 12 katika jimbo la Sichuan, tetemeko ambalo liliuwa watu 70,000 na kujeruhi mamia elfu wengine, na pia kusababisha zaidi ya watu milioni tano kukosa makazi.

Misitu ya dunia itafanyiwa ukaguzi kuinusuru na mabadiliko ya hali ya hewa

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), likishirikiana na nchi wanachama na wadau wengineo kutoka jumuiya kadha wa kadha za kimataifa, wameafikiana kuanzisha upimaji wa hali za misitu iliopo kwenye sehemu zote za ardhi ya dunia yetu, kwa kutumia vifaa vinavyoendeshwa kutokea mbali.

FAO inasema mabadiliko ya hali ya hewa huathiri vibaya uvuvi

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeonya wiki hii kwamba kuongezeka kwa hali ya joto, na mageuzi mengine kwenye mazingira yanayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, ni mambo yatakayoathiri, kwa uzito mkubwa zaidi, uvuvi pamoja na utamaduni wa shughuli za baharini. Kadhalika mabadiliko haya pia hunyima akiba ya chakula fungu maalumu la umma wa kimataifa unaotegemea mavuno ya uvuvi kuishi.

Watalaamu wa UM/UU kuisaidia Philippines kudhibiti uharibifu wa sumu kutoka feri iliozama

Timu ya wataalamu wa UM na Umoja wa Ulaya (UU) hii leo wameelekea Philippines kuitika ombi la Serikali, ili kutathminia viwango vya sumu kali ya kemikali iliomwagika kutoka shehena ya mapipa ya dawa za kuua wadudu, yaliokuwa yamepakiwa kwenye ile feri iliozama karibu na Kisiwa cha Sibuyan, mnamo Juni 21 (2008), baada ya kupigwa na Kimbunga Fengshen.

G8 inalenga kupunguza hewa chafu kwa nusu katika 2050

Viongozi wa Kundi la G8, ambalo huwakilisha mataifa yenye maendeleo makubwa ya viwandani duniani, wameafikiana kupunguza kwa asilimia 50 umwagaji wa hewa chafu angani itakapofika 2050. Ahadi hiyo ilitolewa kwenye majadiliano yanayofanyika kwenye kisiwa cha Hokkaido, Ujapani. Maafikiano haya yanadaiwa yatasaidia udhibiti bora wa athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

BK linajadilia mabadiliko ya hali ya hewa kwa nchi dhaifu

Baraza Kuu (BK) la UM linakutana kujadilia masuala yanayohusu athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwenye nchi dhaifu na masikini, hususan yale mataifa ya visiwa vidogo vidogo.

UM kuonya, rasilmali ya ardhi inaendelea kuchafuliwa, kwahitajika uangalizi bora

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetangaza kwamba kutokana na utafiti wa miaka 20 imebainika kwamba mali ya asili ya ardhi, katika sehemu nyingi za dunia, inaendelea kuharibiwa na kuharibika kwa nguvu na kasi kubwa.

UNEP inasema uwekezaji wa nishati safi ulimwenguni ulikithiri 2007

Achim Steiner, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) ameripoti ya kuwepo uwekezaji mkubwa wa nishati zenye matumizi ya mara kwa mara katika sehemu mbalimbali za dunia, katika kipindi cha karibuni.