Watu jamii ya Maasai huko Loliondo, wilaya ya Ngorongo, Tanzania ambao kwa miaka yote ya uwepo wao shuguli yao ya kujipatia kipato na chakula ni kupitia mifugo hususani ng’ombe, na chakula chao ni nyama na maziwa, sasa wameanza kulazimika kuanza kuhamia katika shughuli za kilimo baada ya shughuli yao hiyo ya asili ufugaji kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.
Zaidi ya watu 45,000 wakiwemo wanawake na watoto 23,000, huenda wakahitaji msaada wa kibinadamu baada ya kimbunga kupiga majimbo ya Nampula, Zambezia, Tete, Niassa, Sofala na Manica nchini Msumbiji tarehe 24 januari 2022.
Timu ya wanasayansi iliyokuwa imetumwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni kufanya utafiti baharini imebaini moja ya miamba nadra na kubwa zaidi wa matumbawe karibu na Tahiti huko bahari ya Pasifiki.
Shirika la hali ya hewa duniani WMO limetoa ripoti ya hali ya hewa ya mwaka 2021 na kueleza kuwa mwaka huo bado ulikuwa moja kati ya miaka saba yenye joto zaidi katika rekodi.
Takriban watu watatu wamefariki dunia nchini Tonga kufuatia mlipuko mkubwa wa volkano na wimbi la Tsunami lililotokea mwishoni mwa wiki. Nyumba na majengo mengine kote kwenye visiwa yamepata uharibifu mkubwa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amehutubia mkutano wa Jukwaa la uchumi duniani, WEF na kuwaeleza viongozi wa sekta ya biashara wanaoshiriki kuwa kinachokosekana hivi sasa duniani ni mshikamano wa kimataifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza kusikitishwa sana na taarifa kuwa Tsunami na majivu vimeathiri nchi ya Tonga, na kwamba tahadhari ya uwezekano wa nchi nyingine kuathirika imetolewa.
Wiki tatu baada ya kimbunga Odette kinachofahamika kimataifa kwa jina Rai kuharibu eneo kubwa la nchi ya Ufilipino, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP kupitia taarifa yake iliyotolewa hii leo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Manila, limeonya kwamba lishe na uhakika wa chakula viko hatarini katika jamii zilizo katika maeneo yenye hali ngumu ikiwa mahitaji ya haraka ya chakula hayatawafikia katika kipindi cha miezi sita ijayo.