Tabianchi na mazingira

Wafugaji Turkana Kenya walazimika kuwa wavuvi:IOM

Wafugaji wa muda mrefu wanaoshi katika pwani ya ziwa Turkana nchini Kenya wanabadilika na kuwa wavuvi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kuwalazimu kubadili mfumo wa maisha .

Mabadiliko kwenye kilimo lazima kupunguza gesi chafu:Cancun

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala ya haki ya kupata chakula ameonya kuwa bila kuwepo kwa hatua madhubuti viwango vya gesi inayochafua mazingira vinavyotokana na kilimo vinatarajiwa kuongezeka kwa asilimia hamsini ifikapo mwaka 2030.

Afrika iko hatarini kupoteza vyanzo vya maji:UNEP

Utafiti mpya ulioangazia hali ya upatikanaji wa maji safi ya kunywa umetaja changamoto zinazozikabili nchi nyingi za afrika kushindwa kusambaza maji kwenye maeneo mbalimbali.

Shirika la UN HABITAT latabiri kuongezeka kwa watu Afrika

Ripoti mpya ya shirika la makaazi la Umoja wa Mataifa UN HABITAT inaonyesha kuwa idadi ya watu kwenye miji ya bara la afrika huenda ikaongezeka mara tatu zaidi kwa muda wa miaka 40 inayokuja.

Hali mbaya nchini Pakistan baada ya mafuriko: UNICEF

Ujumbe wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF uliozuru maeneo ya Shadatkot na Sindh nchini Pakistan kati ya tarehe 21 na 23 mwezi huu unasema kuwa maneo ya vijiji ya sehemu hizo yameharibiwa kabisa huku wanaorejea makiwa wakikosa nyumba , chakula , shule au njia zozote za kujikimu kimaisha kufuatia mafuriko makubwa yaliyoyakumba maeneo hayo. Hadi leo UNICEF imepokea dola milioni 169 kati ya ya dola milioni 251 ilizoomba. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF:

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

Hali ya upatikanaji maji Afrika yazidi kushuka-UNEP

Ripoti moja imesema kiwango cha upatikanaji maji kwa kila mtu barani Afrika kimeanza kushuka.

Familia za wanyama nchini Marekani na Ulaya kwenye hatari ya kuangamia

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO limeonya kuwa huenda familia za wanyama kwa matumizi ya binadamu na kwa kilimo zikatoweka hususan nchini Marekani na barani Ulaya.

WMO na gesi zinazochafua mazingira

WMO inasema kuwa viwango hivyo vimepanda zaidi hata baada ya hali mbaya ya uchumi kuikumba dunia .

Waathirika wa mafuriko Pakistan wahofia majira ya baridi:ICRC

Maelfu ya waathirika wa mafuriko ya Pakistan kwenye jimbo la Khyber Pakhtunhkwa wanakimbizana na wakati kabla ya kuwasili kwa majira ya baridi, hasa kujenga upya nyumba zao, kuondoa mabaki ya uharibifu wa mafuriko na kupanda mazao.

Meya wa Mexico City achaguliwa kuongoza harakati za UM kukabili majanga

Bodi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na uratibu wa upungazaji wa majanga duniani imetangaza mayor wa Mexico City, Marcelo Ebrard, kuwa mjumbe wake maalumu atayeongoza harakati za kuyaandaa majiji kuwa tayari kwa majanga.