Tabianchi na mazingira

Ban ameyataka mataifa tajiri kutimiza ahadi zake kwa mataifa masikini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyatolea wito mataifa tajiri kutimiza ahadi ya kuzifadhili nchi zinazoendelea katika juhudi zake za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mfumo bora wa kilimo utasaidia katika kupunguza tatizo la chakula:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika haki ya chakula, Olivier De Shutter amesema serikali na mashirika ya kimataifa yaanahitaji kuboresha mifumo ya kilimo haraka ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kuokoa mazingira.

Ujenzi mpya baada ya kimbunga Nargis una hatihati Myanmar:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema miaka miwili baada ya Myanmar kukumbwa na kimbunga Nargis kilichouwa watu 140,000 na kuwaacha wengine milioni 3 bila makao, juhudi za kuwasaidia watu hao na ujenzi mpya ziko katika hatihati kutokana na ukosefu wa fedha.

Uwekezaji kwa wasiojiweza ni muhimu kwa uchumi na kutimiza malengo ya milenia:UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa nchi zilizoendelea kiviwanda na mataifa yanayoendelea kujikita katika maendeleo, uchumi unaojali mazingira na mahitaji ya wsiojiweza katika mikakati ya kuchipua uchumi.

Kukabiliana na mmomonyoko wa udogo ni muhimu kwa maisha ya binadamu: UM

Leo ni siku ya kukabiliana na tatizo la ukame duniani na maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza haja ya kuyatunza maeneo makavu ambayo ni makazi ya watu masikini zaidi ya bilioni moja na ambako kuna changamoto kubwa ya kufikia malengo ya maendeleo.

Mahojiano na Lawrence Ndambuki kuhusu hamasa kwa vijana kulinda mazingira

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kuwahamasisha vijana kutoka vyuo vikuu duniani kuhusiana na maswala ya mazingira umefanyika mjini New York.

Ban amesisitiza kutimiza malengo ya milenia barani Afrika

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye anaendelea na ziara barani Afrika amessisitiza umuhimu wa kutimiza malengo ya milenia.

Leo ni siku ya kimataifa ya bahari, umuhimu na uhifadhi wake

Leo ni siku ya kimataifa ya bahari, uhifadhi na umuhimu wake,kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa "bahari zetu, fursa na changamoto".

Vijana Afrika wamewataka viongozi wa dunia kujitahidi kulinda bayo-anuai

Vijana kutoka kote barani Afrika siku ya mazingira wametoa wito kwa viongozi wa dunia kuchukua hatua sasa kulinda bayo-anuai.

Wakati siku ya mazingira ikiadhimishwa UM unachagiza kuhusu bayoanuai

Kila mwaka Mai tano huadhimishwa siku ya mazingira duniani ,kauli mbiu ya mwaka huu ni "viumbe vingi, dunia moja na mustakhbali mmoja".