Tabianchi na mazingira

IAEA inaashiria kukithiri matumizi ya nishati ya nyuklia miaka ijayo

Yury Sokolov, Mkuu wa Idara inayohusika na Nishati ya Nyuklia na pia Naibu Mkurugenzi wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA), amenakiliwa akiashiria kwamba itakapofika 2030 matumizi ya mitambo ya nishati ya nyuklia ulimwenguni itaongezeka kwa asilimia 60.

Kilimo cha kudumu ndio kinga dhidi ya kutanda kwa majangwa, IFAD imeonya

Tarehe 17 Juni huadhimishwa kimataifa kuwa ni Siku ya Kupambana na Ukame na Kutanda kwa Majangwa Duniani. Shirika la UM la Mfuko wa Kimataifa juu ya Maendeleo ya Kilimo (IFAD) limeripoti ya kuwa tatizo la mmomonyoko wa ardhi na kutanda kwa majangwa ni janga lenye kuumiza zaidi kihali wakulima masikini pamoja na wachungaji kwenye maeneo husika. Kwa hivyo IFAD imependekeza hali hiyo irekibishwe, na ilitilia mkazo kwamba tatizo la ukame na kutanda kwa jangwa linaweza kudhibitiwa kwa mfanaikio pindi nchi husika zitakaposhiriki kwenye uekezaji kwenye sekta muhimu ya kilimo, na kwa ushirikiano thabiti na taasisi za kimataifa.~

UNEP imewasilisha mradi mpya wa kuimarisha mazingira ya Nairobi

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limetangaza mradi mpya uliokusudiwa kuimarisha mazingira ya mji mkuu wa Nairobi, Kenya kwa ushirikiano na serikali, baraza la mji, wahisani wa kimataifa na vile vile Shirika la UM juu ya Makazi (UN-HABITAT).

Mchango wa makampuni ya kibinafsi kudhibiti mazingira unasailiwa na UM

Asubuhi pia Baraza Kuu la UM lilifanyisha mjadala wa hadhara kuzingatia jukumu la uekezaji wa makampuni ya kibinafsi, kimataifa, katika kupiga vita athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

UM unaadhimisha Siku ya Kuhifadhi Mazingira Duniani

Tarehe 05 Julai huadhimishwa kila mwaka na jamii ya kimataifa kuwa ni siku ya kukumbushana umuhimu wa hifadhi bora ya mazingira ulimwenguni. Muktadha wa mwaka huu kuiheshimu siku hiyo unatilia mkazo kwa umma wa kimataifa kujiepusha na vitendo vinavyotokana na utumiaji wa nishati yenye kutoa hewa chafu angani, ambayo huharibu mazingira ulimwenguni.

Mazungumzo ya udhibiti wa athari za hali ya hewa duniani yaanzishwa Bonn

Leo mjini Bonn, Ujerumani kumefunguliwa mkutano wa wiki mbili wa UM kuzingatia hatua za kuchukuliwa kipamoja, kuandaa taratibu za kudhibiti bora tatizo la uharibifu unaoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Utunzaji wa viumbe anuwai unahimizwa na UM kwa natija za wote kimataifa

KM Ban Ki-moon na Raisi wa Baraza Kuu Srgjan Kerim wametoa onyo la pamoja wiki hii lenye kutahadharisha kwamba bila ya walimwengu kutunza mazingira ya viumbe na uhai anuwai, matokeo yake yatasababisha athari mbaya kimaisha, hali ambayo itaharibu na kuchafua pakubwa shughuli za uchumi, huduma za maendeleo na zile juhudi za kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa, takriban kote ulimwenguni. Onyo hili liliwasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira, Achim Steiner, kwa niaba ya KM na Raisi wa Baraza Kuu kwenye mkutano wa kusailia sera za kutunza kipamoja viumbe anuwai, unaofanyika mjini Bonn, Ujerumani.

UNEP imependekeza miti bilioni 7 ioteshwe duniani kuhifadhi mazingira

Achim Steiner, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) alipokutana na waandishi habari wa kimataifa hapa Makao Makuu Ijumanne, alitangaza kuanzishwa kampeni mpya iliokusudiwa kuuhamasisha umma wa kimataifa kupandisha miti bilioni 7 katika miezi 18 ijayo.

Dokezo ya kikao cha kuzingatia haki za wenyeji wa asili

Kuanzia tarehe 21 Aprili wajumbe 3,000 ziada waliowakilisha zile jamii zijulikanazo kama wenyeji wa asili, kutoka katika kila pembe ya dunia, walikusanyika hapa Makao Makuu kuhudhuria kikao cha mwaka, cha saba ambacho KM wa UM Ban Ki-moon alikiita \'kikao cha kihistoria kilichofikia njia panda\'. Majadiliano ya mkutano wa wenyeji wa asili yalichukua wiki mbili, na yanatazamiwa kukamilishwa Ijumaa ya leo.

Hapa na Pale

Mkutano wa Saba wa Tume ya Kudumu ya Wenyeji wa Asili umeingia kwenye wiki ya pili ya majadailiano katika Makao Makuu, ambapo masuala yanayotiliwa mkazo zaidi ni yale yanayoambatana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa umma wa kimataifa.