Tabianchi na mazingira

Wajumbe wa kimataifa wakusanyika Poland kuzingatia udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa

Mawaziri wa mazingira na wawakilishi wa ngazi za juu wa kiserikali, kutoka karibu nchi 200, wamekusanyika Alkhamisi ya leo kwenye mji wa Poznan, Poland kuhudhuria kikao cha kuzingatia hatua za kimataifa, za kuharakisha maafikiano ya pamoja, yatakayotumiwa kudhibiti bora matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Wajumbe wa kimataifa waanza mazungumzo rasmi Poznan, Poland kuandaa mkataba mpya wa kuhifadhi mazingira

Katika mji wa Poznan, Poland leo kumeanza majadiliano ya wiki mbili, yanaongozwa na UM, kwenye Mkutano wa Mataifa Yalioridhia Mkataba wa Kudhibiti Bora Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani, ambao makusudio yake hasa ni kuandaa maafikiano ya kusailiwa kwenye Mkutano Mkuu ujao, utakaofanyika 2009 kwenye mji wa Copenhagen, Denmark.