Tabianchi na mazingira

Kemikali tatu zazingatiwa kuchungwa kimataifa

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) imeripoti kwamba kuanzia wiki ijayo maofisa wa kimataifa kutoka serikali 120 ziada watakutana mjini Roma, Utaliana kujadiliana kama aina [mbili] za kemikali zinazotumiwa hivi sasa ulimwenguni ziingizwe kwenye ile orodha inayojulikana kama Orodha ya PIC.

Mafuriko Kenya yahitajia misaada ya kimataifa, inasema OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba nchini Kenya, katika wilaya ya Mandera, mvua kali zilizonyesha huko karibuni zilisababisha ukingo wa mto kubomoka na kuzusha mafuriko yalioathiri zaidi ya kaya 1,000.

Mashirika ya biashara na Umoja wa Mataifa wanazingatia kipamoja utunzaji wa hali ya hewa

Wawakilishi kutoka mashirika makuu ya biashara 150, ikijumlisha pia wajumbe wa jumuiya za kiraia na serikali kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika Ijumanne ya leo Geneva kwenye mkutano unaoungwa mkono na UM, kusailia suluhu za kutoka wafanyabiashara zitakazotumiwa kupambana na matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa yanayopaliliwa na uharibifu wa mazingira.

ITER, IAEA wametiliana sahihi mkataba wa kuimarisha umeme unaotokana na myeyungano wa kinyukilia

Shirika la UM juu ya Matumizi ya Aamani ya Nishati ya Nyklia (IAEA) na Shirika la Kimataifa la Majaribio ya Nishati Nukliajoto (ITER) LEO yametiliana sahihi makubaliano ya kushirikiana kwenye ile miradi ya myeyungano wa kinyuklia utakaozalisha nishati ya umeme kwa wingi.

Mkuu wa IAEA asema shirika limefikia "Njia Panda" kikazi, lahitaji misaada maridhawa kuendesha shughuli zake

Ijumatatu, tarehe 29 Septemba (08) Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) lilianzisha rasmi mkutano wa mwaka, uliohudhuriwa na wawakilishi kutoka Mataifa Wanachama 145. Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Mohamed ElBaradei alisema kwenye hotuba yake ya ufunguzi, na ninamnukuu hapa, “hali ya kazi katika IAEA hairidhishi na sio nzuri.”